Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Gharama za uagizaji chakula duniani kufikia dola trilioni 2 kutokana na kupanda kwa bei:FAO 

Mnunuzi akichagua matunda kwenye soko la Barcelona, ​​Uhispania. Picha: FAO/Alessia Pierdomenico
FAO/Alessia Pierdomenico
Mnunuzi akichagua matunda kwenye soko la Barcelona, ​​Uhispania. Picha: FAO/Alessia Pierdomenico

Gharama za uagizaji chakula duniani kufikia dola trilioni 2 kutokana na kupanda kwa bei:FAO 

Ukuaji wa Kiuchumi

Gharama ya kimataifa ya uagizaji chakula kutoka nje chakula inakadiriwa kupanda hadi dola za Marekani trilioni 1.94 mwaka huu 2022, zaidi ya ilivyotarajiwa hapo awali, kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO. 

Utabiri huo mpya ulioainishwa katika mtazamo wa chakula wa FAO umedhihirisha kiwango cha juu zaidi na ongezeko la asilimia 10 zaidi ya kiwango kilichoweka rekodi cha mwaka 2021, ingawa kasi ya ongezeko hilo inatarajiwa kupungua kutokana na ongezeko la bei ya juu ya chakula duniani na kushuka kwa thamani ya sarafu dhidi ya dola ya Marekani.  

Sababu zote hizo mbili zinapima uwezo wa kununua wa nchi zinazoagiza chakula na, baadaye, kiwango cha chakula kinachoagizwa kutoka nje. 

Ongezeko kubwa linachangiwa na nchi zilizoendelea 

Wanawake wakiwa wamekaa juu ya magunia ya mchele na mahindi huko Wajir, Kenya
FAO/Ami Vitale
Wanawake wakiwa wamekaa juu ya magunia ya mchele na mahindi huko Wajir, Kenya

Sehemu kubwa ya ongezeko la gharama hizo linachangiwa na nchi zenye mapato ya juu, kutokana na bei ya juu zaidi duniani, huku viwango hivyo pia vikitarajiwa kupanda.  

Makundi ya nchi zilizo katika mazingira magumu kiuchumi yanaathiriwa zaidi na bei ya juu.  

Kwa mfano, gharama za jumla uagizaji wa chakula kwa kundi la nchi za kipato cha chini unatarajiwa kubaki bila kubadilika ingawa unatabiriwa kupungua kwa asilimia 10 katika suala kiwango cha uagizaji, ikiashiria kuongezeka kwa suala la ufikiaji wa chakula hicho kwa nchi hizi. 

"Hizi ni dalili za kutisha kulingana na mtazamo wa uhakika wa chakula, zinaonyesha waagizaji wanapata ugumu wa kufadhili kupanda kwa gharama za kimataifa, na hivyo kuashiria mwisho wa kustahimili bei ya juu ya kimataifa," imeonya ripoti hiyo kutoka kitengo cha masoko na biashara cha FAO. 

Pengo lililopo kuongeza athari 

Ripoti hiyo ya mtazamo wa chakula, ambayo inaainisha mifumo ya biashara ya chakula na makundi ya chakula, inaonya kwamba tofauti zilizopo zinaweza kuwa mbaya zaidi, huku nchi zenye mapato ya juu zikiendelea kuagiza bidhaa za chakula kutoka kwa wigo mzima wa bidhaa za chakula, wakati kanda zinazoendelea zikizingatia vyakula vikuu pekee.  

Katika muktadha huu, FAO inakaribisha idhini ya shirika la fedha duniani IMF ya upenyo wa mshtuko wa Chakula kwa msingi wa pendekezo la FAO la usaidizi wa ufadhili wa uagizaji wa chakula kama hatua muhimu ya kupunguza mzigo wa kuongezeka kwa gharama za uagizaji wa chakula miongoni mwa nchi za kipato cha chini.
Ununuzi wa bidhaa zingine ikiwemo mbolea umepigwa jicho 

Bei ya chakula inaathiri maisha ya wakulima na watumiaji
FAO
Bei ya chakula inaathiri maisha ya wakulima na watumiaji

Ripoti hiyo ya mtazamo wa chakula pia imetathmini matumizi ya kimataifa kwa bidhaa kama pembejeo za kilimo zinazoagizwa kutoka nje, ikiwa ni pamoja na mbolea.  

Gharama za kimataifa za uagizaji wa pembejeo zinatarajiwa kupanda hadi dola za Marekani bilioni 424 mwaka 2022, hadi kufikia asilimia 48 kutoka mwaka uliopita na kiasi cha asilimia 112 kutoka mwaka 2020. 

Gharama za juu za nishati na mbolea zinazoagizwa kutoka nje ndio chachu ya  ongezeko lililotarajiwa la bei ya chakula.  

Bidhaa hizo mbili zianachangia hasa gharama za kuagiza, na kusababisha matatizo yanayoonekana sasa kwa nchi za kipato cha chini na za chini na kipato cha kati.  

Na matokeo yake , baadhi ya nchi zinaweza kulazimika kupunguza maombi ya pembejeo, kna hivyo kutoepuka kusababisha uzalishaji mdogo wa kilimo na upatikanaji mdogo wa chakula cha ndani.  

"Athari mbaya kwa pato la kilimo duniani na uhakika wa chakula huenda zikaendelea hadi mwaka 2023”, kulingana na FAO.