Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampeni ya #IBelong yafikisha miaka 8 utashi wa kisiasa wahitajika kufanikisha

Serikali ya Kenya imetoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto 600 kutoja jamii ya Washona, ikiwa ni hatua muhimu ya kuwalinda na hatua ya kwanza kuelekea kumaliza tatizo la utaifa kwa watu 3,500 nchini humo.
UNHCR KENYA/Rose Ogolla
Serikali ya Kenya imetoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto 600 kutoja jamii ya Washona, ikiwa ni hatua muhimu ya kuwalinda na hatua ya kwanza kuelekea kumaliza tatizo la utaifa kwa watu 3,500 nchini humo.

Kampeni ya #IBelong yafikisha miaka 8 utashi wa kisiasa wahitajika kufanikisha

Wahamiaji na Wakimbizi

Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, Filippo Grandi ametoa wito wa utashi wa kisiasa katika kujitolea zaidi kuboresha maisha ya takriban watu milioni 4.3 wasio na utaifa duniani kote ambao "wanataabika bila uraia na wanaoishi katika vivuli."

Katika taarifa iliyotolewa leo na UNHCR iliwa ni maadhimisho ya miaka nane ya kampeni ya #I Belong au #Miminiwa, inayoendeshwa na shirika hilo ikilenga kukomesha ukosefu wa uraia imemnukuu Grandi akisema kuwa Kutokuwa na utaifa ni “ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, pamoja na doa kwa ubinadamu”.

Kamishna Grandi ameongeza kuwa “Kwa kunyimwa haki ya msingi ya utaifa, wale ambao wamezaliwa au kuachwa bila utaifa wanakabiliwa na mkanganyiko mkubwa wa kisheria. Wanazuiwa kupata haki zao za kimsingi za kibinadamu na kushiriki kikamilifu katika jamii. Maisha yao yana alama ya kutengwa, kunyimwa, na kutengwa.

Sisi sote ni wa mahali

Mkuu huyo wa UNHCR alitoa ombi la kukomesha kutokuwa na utaifa ndani ya muongo mmoja, au ifikapo mwaka 2024.

Ametaja pia kuna maendeleo yamefanywa ambapo takriban watu 450,000 wasio na utaifa ama wamepata utaifa au wamethibitishwa utaifa wao.

Zaidi ya hayo, makumi ya maelfu ya watu kutoka Barani Asia, Ulaya, Afrika na Amerika sasa wanamwelekeo wa kupata uraia kutokana na mabadiliko mapya ya sheria.

Kwa hakika sasa na mimi naishi

Ingawa watu wengi pengine wanachukulia uraia wao kuwa jambo la kawaida, kutokuwa na karatasi kunaweza kufanya maisha kuwa magumu jambo ambalo Linda, ambaye sasa ana umri wa miaka 30, amekuwa akiliishi katika kipindi cha maisha yake yote.

Linda alizaliwa huko Moscow, lakini hakuwa na uraia wa Urusi. Mama yake, ambaye alikuwa anatoka Mashariki ya Kati, alikuwa amekuja nchini humo kusomea uandishi wa habari. Kwa sababu hakuwa na utaifa, Linda alikuwa na hadhi sawa na mama yake.

Bila karatasi, Linda hangeweza kufungua akaunti ya benki, kukodisha nyumba, au hata kununua kadi ya simu yake.

“Mnamo Novemba 10, 2018, nilipokea barua ya taarifa kwamba nimepewa uraia wa Urusi. Ilikuwa wakati wa hisia sana … nilihisi kwamba sasa naishi ” aliiambia UNHCR katika mahojiano, miaka kadhaa baada ya kuwa raia.

 

Tatizo la kimataifa, suluhu za kitaifa

Shirika hilo la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na masuala ya wakimbizi liliripoti kuhusu hatua kadhaa pamoja na masuluhisho mengine mengi waliyofanikiwa kuyafikia tangu kampeni ya #Ibelong ilipozinduliwa.

Nchi tatu zimerekebisha sheria za utaifa zenye ubaguzi wa kijinsia kama sababu kuu ya kutokuwa na utaifa.

Hata hivyo, serikali 24 zinaendelea kuwanyima haki sawa wanawake kutoa utaifa kwa watoto wao, kwa misingi sawa na wanaume.

Zaidi ya hayo, maendeleo ya kumaliza ukosefu wa utaifa yanaendelea kuibuka dhidi ya vikwazo vingine, UNHCR ilisema, mara nyingi hutokana na ubaguzi wa rangi, dini au kabila.

"Wakati ukosefu wa utaifa unasalia kuwa tatizo la kimataifa, na sababu nyingi tofauti, lakini ni suala ambalo linaweza kutatuliwa kupitia, mara nyingi rahisi sana, ufumbuzi wa ndani," alisema Grandi.

"Ninatoa wito kwa serikali na wabunge kote ulimwenguni kutumia miaka miwili ijayo ya kampeni hii kuharakisha hatua na kuziba mapengo ya kisheria na kisera ambayo yanaendelea kuwaacha nyuma mamilioni ya watu.