Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kufungwa kwa hospitali ya Mada Cameroon ni kuwanyima raia huduma ya afya- UN

Mwanamke akiwa na wajukuu wake watatu baada ya kusajiliwa katika kituo cha mapokezi ya wakimbizi kutoka Cameroon huko Oundouma  nchini Chad
© UNHCR/Aristophane Ngargoune
Mwanamke akiwa na wajukuu wake watatu baada ya kusajiliwa katika kituo cha mapokezi ya wakimbizi kutoka Cameroon huko Oundouma nchini Chad

Kufungwa kwa hospitali ya Mada Cameroon ni kuwanyima raia huduma ya afya- UN

Amani na Usalama

wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu nchini Cameroon, Olivier Beer ameeleza hofu yake juu ya athari za kufungwa kwa muda usiojulikana kwa  hospitali ya Mada huko mkoa wa Far KAskazini nchini Cameroon baada ya shambulizi la tarehe Pili mwezi huu wa julai kutoka kundi la watu waliokuwa wamejihami. 

Taarifa iliyotolewa hii leo na ofisi ya mratibu huyo kwenye mji mkuu wa Cameroon, Yaoundé, imemnukuu Bwana Beer akisema hospitali hiyo ndio pekee inayotegemewa na wenyeji,  wakimbizi na wakimbizi wa meneo ya mpakani ya Nigeria na Chad hivyo kufungwa kwake kunaweza kuwanyima watu hao haki ya msingi ya kupata huduma ya afya. 

Wakati wa shambulio hilo, raia mmoja aliuawa na sasa hospitali imefungwa ingawa ina vifaa muhimu vya matibabu kwa majeruhi.

Kufuatia kufungwa kwa hospitali hiyo, raia wanaohitaji tiba ya upasuaji wa dharura watalazimika kusafiri hadi Kousseri au kuvuka mpaka kwenda mji mkuu wa Chad, Nd’Jamena, mji ambao ni kilometa 100 kutoka Mada.

Ukosefu wa usalama ni mateso kwa raia

Eneo la wilaya za Logone na Chari kwenye mkoa wa Far Kaskazini hukumbwa na ghasia za mara kwa mara na hazina  usalama wa kutosha, halikadhalika miundombinu ya barabara ni mibovu  hususan msimu wa mvua na hivyo kufanya hali kuwa ngumu zaidi katika kusafirisha raia wanaojeruhiwa kwenye mashambulizi.

Ni kwa mantiki hiyo, Mratibu huyo wa  analaani vikali shambulio hilo kwa kuwa “huduma za afya ni vituo muhimu sana vya kuokoa maisha ya wakazi wa mkoa wa Far Kaskazini.

“Watoto, wanawake na wanaume wanahitaji huduma za afya,” amesema Bwana Beer akiongeza kuwa “mashambulizi dhidi ya vituo vya afya, wahudumu wa afya, na wagonjwa ni ukiukwaji wa haki za kibinadamu na haki za masuala ya kibinadamu. Pande zote kwenye mzozo zina wajibu wa kuheshimu na kulinda wahudumu wa afya, maeneo ya vituo vya afya pamoja na magari, majeruhi na wagonjwa.”

TAGS: Cameroon, Far Kaskazini, Mada, Olivier Beer, Haki za binadamu