Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali inazidi kuwa mbaya Yemen: OCHA

Msichana wa Yemen mwenye umri wa miaka 12 na mdogo wake wa kiume
© UNICEF/Areej Alghabri
Msichana wa Yemen mwenye umri wa miaka 12 na mdogo wake wa kiume

Hali inazidi kuwa mbaya Yemen: OCHA

Msaada wa Kibinadamu

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Naibu Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA Joyce Msuya amesema  janga la kibinadamu nchini Yemen linakaribia kuwa baya zaidi. 

Akizungumza katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani Msuya amesema ijapokuwa kuna makubaliano yamefikiwa nchini humo lakini hayatoshi kuzuia kunachohofiwa kutokea katika wiki na miezi michache ijayo ambacho ni mahitaji ya kibinadamu nchini kote na hatari ya njaa katika baadhi ya maeneo. 

Mkuu huyo wa ofisi ya OCHA amesema jumuiya ya kimataifa lazima ichukue hatua za haraka na madhubuti kukomesha hatari inayokuja na kutaja mambo kadhaa yanayoweza kufanyika kwa sasa ili kusaidia wananchi wa Yemen.

“Katika muhtasari wa tarifa tuliyotoa wiki chache zilizopita tulionya juu ya kuongezeka kwa mahitaji (ya kibinadamu) kutokana na changamoto za kiuchumi, kuzidi kuzorota kwa mazingira ya wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu na kuporomoka kwa ufadhili wa misaada ya kibinadamu.”

Msuya amefafanua namna fecha ya nchi hiyo ilivyoshuka thamani na inavyoshindwa kukidhi mahitaji ya muhimu ya kibinadamu kama vile chakula kwakuzingatia pia kupanda kwa gharama za chakula duniani kutokana na vita inayoendelea nchini Ukraine. 

Ameshukuru pia nchi ambazo zilijitoa kwa haraka kusaidia kukabiliana na dharura inayowakabili wananchi wa Yemen

“Mwezi April Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu UAE zilitangaza kuisaidia Yemen kwakutoa dola bilioni 3 ili kukabiliana na changamoto za kiuchumi… fedha hii ikitolewa itasaidia kuleta utulivy wa anguko la kiuchumi ambalo linachocheea kupanda kwa njaa na mahitaji mengine” amesemMsuya huku akahamasisha fedha hinahitajika kutolewa kwa haraka huku akigusia pia majadiliano ya msaada wa ngano ambao India inataka kutoa kwa Yemen. 

Joyce Msuya, Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Masuala ya Kibinadamu na Naibu Mratibu wa Misaada ya Dharura akitoa maelezo kwa mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu hali ya Yemen.
UN Photo/Manuel Elías
Joyce Msuya, Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Masuala ya Kibinadamu na Naibu Mratibu wa Misaada ya Dharura akitoa maelezo kwa mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu hali ya Yemen.

Watoa huduma 

Suala lingine lililozungumza katika Baraza la Usalama ni kuhusu usalama wa wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu nchini Yemen ambapo watoa misaada wamekuwa wakikabiliana na changamoto na vitisho hali inayoelezwa kuchochewa na Habari potofu zinazoenezwa kupitia mitandao ya kijamii, meseji za kawaida za sim una majukaa ya umma. 

“Katika maeneo yanayoshikiwa na Houthi, shughuli za wafanyakazi (wa misaada ya kibinadamu) zimekuwa ngumu zaidi hivi karibuni kutokana na vikwanzo vitokanavyo na ukiritimba kwa wafanyakazi ambao ni raia wa Yemen wanaosafiri kwenda nje ya nchi kwa sababu za kitaalamu.” 

Mkuu huyo wa OCHA ameongeza kuwa “Mamlaka ya Houthi wanazidisha vikwazo vinavyowabana wanawake kushiriki katika masuala ya kibinadamu – kama wafanyakazi wa misaada na kama wapokea misaada ya kininadamu.”

Amekumbusha pia ikiwa imepita miezi minane tangu kuwahimiza maafisa wa usalama huko Sana’a kuwaachia wafayakazi wawili wa Umoja wa Mataifa, kitendo ambacho ni ukiukaji wa kinga kwa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa.