Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jukumu la kusaidia wanawake wa Taliban ni letu sote: Bachelet

Wanawake katika chumba cha kusubiri kuhudumiwa katika kiliniki nchini Afghanistan
© UNICEF/Alessio Romenzi
Wanawake katika chumba cha kusubiri kuhudumiwa katika kiliniki nchini Afghanistan

Jukumu la kusaidia wanawake wa Taliban ni letu sote: Bachelet

Wanawake

Umoja wa Mataifa umeusihi uongozi wa Taliban kukubali ombi la wanawake wanchi hiyo la kukaa nao na kujadiliana masuala mbalimbali ikiwemo haki zao za kibinadamu.

Taarifa ya Kamishna Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet kutoka Geneva Uswisi imesema ni vyema uongozi huo ukazungumza na kuchukua uzoefu kutoka katika mataifa mengine yanayofuata sheria za kiislamu huku wakiheshimu haki za binadamu na kufanya hivyo katika taifa lao ili kutozidi kuwadumbukiza wanawake wa taifa hilo katika dimbi la giza.

Mapema mwezi Machi mwaka huu (2022) Kamishna Bachelet alitembelea nchini Afghanistan na kuzungumza na wanawake kutoka sekta mbalimbali ambao ameeleza alivutiwa na namna walivyokuwa wawazi na wakitaka mazungumzo ya moja kwa moja na mamlaka (ya Taliban) na kwamba Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA ndio imechukua jukumu la kuwezesha ombi hilo.

 

Bachelet amesema “Leo nawaomba tena kuitikia wito wa dharura wa wanawake wa kukaa nao kwenye meza ya mazungumzo na kushirikiana kwenye mazungumzo ya maana. Hii itafaidisha Afghanistan kwa ujumla.”

 

Akizungumzia sheria mbalimbali zilizoanzishwa mara tu baada ya Taliban kushika madaraka ikiwa nai Pamoja na katazo la wanawake na wasichana kuendelea na masomi, kufanya kazi au kujiajiri wenyewe Pamoja na kutotembea wenyewe Bachelet amesema “Natoa wito kwa mamlaka (ya Taliban) kuweka tarehe rasmi ya kufunguliwa shule za sekondari za wasichana na kuhakikisha wanapata elimu bora bila ubaguzi na wapewe rasilimali na walimu. Nawasihi pia waondoe vikwanzo vya wanawake kutembea kwa uhuru iliwa ni Pamoja na hitaji la lazima la kufunika uso, wapate haki yao ya kupata ajira Pamoja na kujiajiri wenyewe”

 

Amekumbusha kuwa katika ulimwegu tuliopo wenye mzozo wa kiuchumi, mchango wa wanawake katika shughuli za kiuchumi niwa lazima ambao wenyewe wenyewe unahitaji kupata elimu na uhuru wa kutembea na kutokuwa kwenye vurugu.

 

Jukumu la jumiya za kimataifa

 

Kwanza Bachelet amewashukuru jumuiya ya kiislamu iliyoenda kufanya mazungumzo na uongozi wa Taliban hivi karibuni na kusema ni mwenendo mzuri.

 

Pia amezisihi jumuiya za kimataifa kutowaacha bila kuwasaidia wanawake na wasichana wa Afghanistan ambao haki zao zimezimwa kabisa.

 

“Kwa wanawake wa Afghanistan wakati ujao wanaona giza, labda kutokee mabadiliko tena kwa haraka. Ni jukumu letu sote, kwa pamoja, huku tukiongozwa na wanawake wa Afghanistan mbele lazima tuhakikishe haki za wote wanawake na wasichana zinalindwa na kuheshimiwa.”

 

Amezikumbusha nchi zilizoiwekea vizuizi nchi ya Afghanistan mkuu huyo wa haki za binadamu amesema, “ninaomba zile nchi wanachama ambazo zimeweka vikwazo ili kuwezesha usaidizi unaohitajika kwa watu wenye uhitaji.”

 

Amesisitiza zaidi kuhakikisha haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na haki za wanawake ziwe katikati ya tathmini zote za kibinadamu na programu za usaidizi kwa nchi ya Afghanistan. “Wanawake wanapaswa kuwa na upatikanaji salama na sawa wa misaada ya kibinadamu, ikiwa ni pamoja na upatikanaji usiozuiliwa kwa wafanyakazi wa misaada wa kike.”

 

Bachelet ameituma salamu za pole kwa taifa zima la Aghanistan kwa tetemeko lililowakumba mwezi juni .