Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nimesikitishwa na kuvunjwa kwa tume huru ya haki za binadamu Afghanistan-Bachelet 

Wanawake wawili nchini Afghanistan wakitembea karibu na msikiti wa kale kwenye jimbo la Herat
UNAMA
Wanawake wawili nchini Afghanistan wakitembea karibu na msikiti wa kale kwenye jimbo la Herat

Nimesikitishwa na kuvunjwa kwa tume huru ya haki za binadamu Afghanistan-Bachelet 

Haki za binadamu

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu Michelle Bachelet ametoa taarifa leo akisema amesikitishwa na uamuzi ulioripotiwa wa Taliban kuvunja tume huru ya Haki za Kibinadamu ya nchi hiyo.

"Tume huru ya Haki za Kibinadamu ya Afghanistan, AIHRC imefanya kazi kubwa katika hali ngumu sana kwa miaka mingi, ikiangazia haki za binadamu za Waafghanistan wote, ikiwa ni pamoja na waathirika wa pande zote za mzozo. Hata hivyo, haijaweza kufanya kazi mashinani tangu Agosti 2021," amesema Kamishna Mkuu huyo akibainisha kuwa tume hiyo"imekuwa sauti yenye nguvu kwa haki za binadamu na mshiriki anayeaminika wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, na kupotea kwake itakuwa hatua ya kurudi nyuma kwa Waafghanistan wote na jamii ya kiraia ya Afghanistan. 

Bi Bachelet kupitia taarifa yake amesema mwezi Machi mwaka huu alifanya majadiliano na mamlaka husika kuunda upya mbinu huru ya kufuatilia haki za binadamu ambayo inaweza kupokea malalamiko kutoka kwa umma na kuwasilisha mbele ya mamlaka  masuala yanayoibua wasiwasi.