Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Picha ya kuchora kutoka kwenye maonesho ya 'Unyanyasaji wa Kijinsia katika Migogoro. Youth Speaks Out through the Arts’ iliyoandaliwa na Ofisi ya Mwakilishi Maalum wa Ukatili wa Kijinsia katika Migogoro, ikitazamwa katika Makao Makuu ya UN

Hivi ndivyo tunavyopaswa kusaidia wathaarika wa unyanyasaji wa kijinsia katika maeneo ya vita

screenshot / UN
Picha ya kuchora kutoka kwenye maonesho ya 'Unyanyasaji wa Kijinsia katika Migogoro. Youth Speaks Out through the Arts’ iliyoandaliwa na Ofisi ya Mwakilishi Maalum wa Ukatili wa Kijinsia katika Migogoro, ikitazamwa katika Makao Makuu ya UN

Hivi ndivyo tunavyopaswa kusaidia wathaarika wa unyanyasaji wa kijinsia katika maeneo ya vita

Amani na Usalama

Unyanyasaji wa kijinsia katika maeneo ya vita ni moja ya mbinu ya kivita na ukandamizaji ambayo imeathiri idadi kubwa ya watu, kuharibu maisha yao na kuvunja jamii kwakuwa waathirika wa unyanyasaji huo hubeba mzigo mkubwa wa unyanyapaa, kuathirika kisaikolojia na mara nyingi jamii kuwatupia lawama huku wahalifu mara chache huchukuliwa hatua kwa matendo yao.

Ikiwa leo ni siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Unyanyasaji wa Kijinsia katika maeneo yenye migogoro, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa taarifa yake na kusema “tunasimama kwa mshikamano na walionusurika na kujitolea kusaidia wanawake, wasichana, wanaume na wavulana walio hatarini zaidi wanapojitahidi kuishi kwa utu na amani katikati ya majanga ya kibinadamu.” Amesema shirika hilo analoliongoza linaendelea kujitahidi kuongeza msaada kwa waathiriwa na wanawake waliokimbia makazi yao, wasichana na wavulana ambao wako hatarini kwa usafirishaji haramu wa binadamu na unyonyaji wa kijinsia, na wale kutoka maeneo yaliyotengwa, ya mbali na vijijini ambapo mifumo ya haki na ulinzi ni dhaifu. Guterres ameeleza namna watu wengine wanavyoweza kusaidia waathirika wa kijinsia - Kuimarisha mifumo ya haki ya kitaifa na uwezo wa utawala wa sheria, kwa hivyo wahalifu wanawajibishwa kwa uhalifu wao, na waathiriwa hupokea usaidizi wa matibabu na kisaikolojia kwa wakati. - Kuheshimu na kushikilia haki za waathirika, na kuwatendea kwa heshima na uelewa, huku ikiwapa fursa ya kusaidia kurekebisha jamii zao zilizogawanyika. - Kusaidia mashirika ya kiraia yanayoongozwa na wanawake yanayofanya kazi kuvunja vizuizi vya kijamii, kiuchumi na kitamaduni ambavyo vinawanyima wanawake na wasichana haki zao za kulindwa, usawa na haki. - Kushughulikia sababu za msingi za unyanyasaji wa kijinsia katika migogoro, Kuanzia kwenye usawa, hadi udhaifu wa kitaasisi na kijeshi, na kuimarisha mifumo ya tahadhari ya mapema ili kuzuia uhalifu huu kutokea kwanza. Mkuu huyo wa umoja wa Mataifa amesema kwa kuongezeka kwa azimio la kisiasa na rasilimali za kifedha, “tunaweza kulinganisha maneno na vitendo na kumaliza janga la unyanyasaji wa kijinsia katika migogoro, mara moja na kwa wote.”