Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR imeweka takwimu kwenye tovuti kuonesha usafiri wa wakimbizi wa Ukraine 

Wanawake na watoto wakipanda treni kwenye kituo cha Lviv nchini Ukraine ili kuhamishiwa maeneo mengine yenye usalama,
© UNICEF/Nikita Mekenzin
Wanawake na watoto wakipanda treni kwenye kituo cha Lviv nchini Ukraine ili kuhamishiwa maeneo mengine yenye usalama,

UNHCR imeweka takwimu kwenye tovuti kuonesha usafiri wa wakimbizi wa Ukraine 

Wahamiaji na Wakimbizi

Vita ya Ukraine imesababisha janga kubwa zaidi la uhamishaji wa watu ulimwenguni hii leo. Mamilioni ya wakimbizi wamevuka na kuingia katika nchi jirani, na wengi zaidi wamekimbia makazi yao ndani ya nchi. Limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR ambalo linashughulikia hali kadri takwimu mpya zinavyopopatikana. 

UNHCR imeweka tovuti ambayo inawasilisha makadirio ya idadi ya wakimbizi waliorekodiwa katika nchi 44 kote Ulaya pamoja na masahihisho kuhusu vivuko vya mpakani kutoka Ukraine tangu tarehe 24 Februari, wanaohama kurejea Ukraini na vile vile usajili wa ulinzi wa muda barani Ulaya.  

Kufikia Juni 7, wanaovuka mpaka na kurekodiwa wamefikia  milioni 7.3 kutoka Ukraine, na idadi ya vingine milioni 2.3 wamerekodiwa kuvuka kurejea nchini humo.   

Kulingana na takwimu mpya zilizotolewa na mamlaka za kitaifa na kukusanywa na UNHCR, takriban wakimbizi milioni 4.8 kutoka Ukraine wamerekodiwa kote Ulaya, wakiwemo wale waliovuka kwanza hadi nchi jirani na baadaye kuelekea kwingine.  

"Tangu mwanzo, UNHCR imeimarisha uwezo wake wa ukusanyaji na uchambuzi wa takwimu katika nchi zinazopokea wakimbizi kuhusu wasifu, udhaifu na nia ya wakimbizi," amesema Raouf Mazou, Kamishna Mkuu Msaidizi wa Operesheni wa UNHCR. "Hii ni muhimu ili kuhakikisha mwitikio mzuri wa kibinadamu, unaotuwezesha sisi na wadau kujibu mahitaji muhimu kwa usaidizi maalum, na kupanga mipango bora ya siku zijazo." 

Kuongezeka kwa mshikamano katika Mataifa yanayopokea wakimbizi bado ni jambo la ajabu. Nchi Wanachama wa Umoja wa Ulaya zimechukua hatua ambazo hazijawahi kushuhudiwa, kuwezesha kwa haraka maelekezo ya ulinzi wa muda kwa mara ya kwanza, kuhakikisha upatikanaji wa ulinzi na huduma kwa wakimbizi kutoka Ukraine. Mataifa mengine ya Ulaya yameongeza mipango kama hiyo ya ulinzi. 

Kati ya wakimbizi milioni 4.8 wa Ukraine waliorekodiwa barani Ulaya, milioni 3.2 wamejiandikisha kwa ulinzi wa muda au mipango kama hiyo ya ulinzi wa kitaifa. 

Ingawa hali ya usalama nchini Ukraine bado ni tete, matukio ya kwenda na kurudi yamerekodiwa. Wengine huvuka kwenda Ukraine kutathmini hali, kuangalia mali, kutembelea wanafamilia au kuwasaidia kuondoka. Wengine wanaenda Magharibi mwa Ukraine na maeneo karibu na Kyiv na Chernihiv kwa nia ya kusalia pale. 

Wengi ambao wamerejea nyumabni wamekuta nyumba zao zimeharibiwa vibaya na walihangaika kupata kazi huku vita ikiendelea kuwa na athari mbaya za kiuchumi na hawakuwa na chaguo ila kuondoka tena. Maendeleo haya yameonyeshwa kwenye tovuti iliyosahihishwa.