Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunayo heshima kubwa kwa walinda amani kutokana na kujitolea kwao - Guterres 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres  (kushoto) akishiriki hafla ya kuweka shada la maua kwa ajili ya kuadhimisha siku ya walinda amani ya Umoja wa Mataifa mwaka 2022.
UN Picha/ Mark Garten
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres (kushoto) akishiriki hafla ya kuweka shada la maua kwa ajili ya kuadhimisha siku ya walinda amani ya Umoja wa Mataifa mwaka 2022.

Tunayo heshima kubwa kwa walinda amani kutokana na kujitolea kwao - Guterres 

Amani na Usalama

“Leo, tunayo heshima ya kuwaenzi wanawake na wanaume zaidi ya milioni moja ambao wameshiriki kama walinda amani wa Umoja wa Mataifa tangu mwaka 1948.” Ndivyo alivyoanza Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres katika ujumbe wake wa siku ya kimataifa ya walinda amani. 

Ingawa kwa kawaida siku hii ya walinda amani, huadhimishwa kila tarehe 29 ya mwezi Mei ili kutambua na kuenzi walinda amani kote duniani, hafla ya kuiadhimisha siku hii katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani imefanyika leo.  

Hafla hii imeambatana na Katibu Mkuu Guterres kuweka shada la maua katika eneo maalumu kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa na pia kukabidhi nishani tatu, moja ikiwa ni inayofahamika kama Nishani ya ‘Kapteni Mbaye Diagne - ya Ujasiri wa Kipekee’, nyingine ikiwa ni ya Mchechemzi Bora wa Kijeshi wa Jinsia na nyingine ikiwa ni Nishani ya Dag Hammarskjold. 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres  (katikati) akishiriki hafla ya kuweka shada la maua kwa ajili ya kuadhimisha siku ya walinda amani ya Umoja wa Mataifa mwaka 2022.
UN Photo/Mark Garten
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres (katikati) akishiriki hafla ya kuweka shada la maua kwa ajili ya kuadhimisha siku ya walinda amani ya Umoja wa Mataifa mwaka 2022.

Nishani ya mwaka huu ya ‘Kapteni Mbaye Diagne - ya Ujasiri wa Kipekee’ ametunukiwa Marehemu Kapteni Abdelrazakh Hamit Bahar wa Chad. 

Katika ujumbe wa video uliosambazwa mapema, Katibu Mkuu Guterres akizungumzia walinda amani waliopoteza maisha wakati wa kutekeleza majukumu ameeleza namna Umoja wa Mataifa unavyotambua na kuheshimu mchango wa aliowaita, “mashujaa takribani 4200 wanawake na wanaume ambao wamejitolea maisha yao ili kuleta amani.” 

Aidha Bwana Guterres amesisitiza kuhusu ukweli wa siku nyingi: amani haiwezi kuchukuliwa  kimzaha mzaha. “Amani ni zawadi.” Amesema.  

Mkuu huyo wa UN amesema Umoja wa Mataifa unatoa shukrani kuu kwa walinda amani wapatao 87000 ambao ni raia, polisi, na wanajeshi wanaofanya kazi chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa, ambao wanasaidia   upatikanaji wa zawadi ya amani duniani kote. 

“Wanakumbwa na changamoto kubwa. Ongezeko la vitendo vya ukatili mkubwa dhidi ya walinda amani kumefanya kazi ya Walinda amani kuwa  ngumu zaidi.Vikwazo vilivyotokana na Covid-19 vimefanya kazi kuwa ngumu zaidi Lakini Walinda amani wa Umoja wa Mataifa huendelea kujitolea kwa umahiri kama wadau wa amani. Mwaka huu, tunaangazia nguvu ya ushirikiano.” Amezieleza changamoto za walinda amani akiahidi kuzitatua kwa kuongeza ushirikiano.  

Guterres ameueleza ulimwengu kuwa tunafahamu ya kwamba amani hufanikiwa kupatikana pale ambapo serikali na jamii zinapoungana ili kutatua tofauti kwa njia ya mazungumzo, kujenga utamaduni wa kutokuwa na ukatili na kuwalinda wasiokuwa na uwezo. 

Duniani kote, Walinda amani hufanya kazi na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, Asasi zisizokuwa za kiraia, wanaotoa huduma za kibinadamu, vyombo vya habari, jamii wanazofanyia kazi na wengine ili kuimarisha amani, kulinda raia, kuendeleza haki za binaadamu na utawala wa sheria ili kuboresha maisha ya mamilioni ya watu. 

Mkuu wa UN amehitimisha akisema, “leo na kila siku, tunawaheshimu kwa kujitolea kwao kusaidia jamii kuachana na migogoro, kuelekea kwenye amani na ustawi kwa wote, katika siku zijazo. Tutakuwa daima na deni lao.” 

Kapteni Abdelrazakh(katikati) alitumwa kambi ya wakimbizi ya Aguelhok Kaskazini mwa Mali wakati ilishambuliwa na kundi la kigaidi.
Kwa hisani ya Luteni Kanali Chahata Ali Mahamat
Kapteni Abdelrazakh(katikati) alitumwa kambi ya wakimbizi ya Aguelhok Kaskazini mwa Mali wakati ilishambuliwa na kundi la kigaidi.

 

Nishani kwa walinda amani - Mashujaa

Katika hatua nyingine, hafla hiyo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kuadhimisha siku ya kimataifa ya siku ya walinda amani, imetumika kutoa nishani kwa walinda amani. 

Nishani zilizotolewa ni Nishani ya ‘Kapteni Mbaye Diagne - ya Ujasiri wa Kipekee’, nishani ya Mtetezi Bora wa Kijeshi wa masuala ya kijinsia na Nishani ya Dag Hammarskjold. Nishani ya mwaka huu ya ‘Kapteni Mbaye Diagne - ya Ujasiri wa Kipekee’ ametunukiwa Marehemu Kapteni Abdelrazakh Hamit Bahar wa Chad ambaye aliuawa mwezi Aprili mwaka jana 2021 akiwalinda raia na walinda amani wenzake wakati Kambi ya Aguelhok  nchini Mali iliposhambuliwa na kundi la kigaidi lenye silaha lililojaribu kuteka kambi hiyo na viunga vyake. Katibu Mkuu Guterres ameikabidhi tuzo hiyo kwa baba mzazi wa Marehemu Kapteni Bahar.  

Meja Winnet Zharare kutoka Zimbabwe, mshindi wa tuzo ya Umoja wa Mataifa ya mwanajeshi mtetezi bora wa masuala ya jinsia kwa mwaka 2021.
Kwa hisani ya Meja Winnet Zharare
Meja Winnet Zharare kutoka Zimbabwe, mshindi wa tuzo ya Umoja wa Mataifa ya mwanajeshi mtetezi bora wa masuala ya jinsia kwa mwaka 2021.

Mwingine aliyepokea tuzo yake ni Meja Winnet Zharare, mwenye umri wa miaka 39 mlinda amani raia Zimbabwe ambaye hivi karibuni alimaliza kazi yake katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini UNMISS, yeye amepewa tuzo ya Umoja wa Mataifa ya mwanajeshi mtetezi bora wa masuala ya jinsia kwa mwaka 2021.