Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa pamoja wa UNESCO, UNFPA na UN Women, mkombozi kwa vijana Tanzania 

Mwanafunzi akiwa darasani
UNICEF TANZANIA
Mwanafunzi akiwa darasani

Mradi wa pamoja wa UNESCO, UNFPA na UN Women, mkombozi kwa vijana Tanzania 

Utamaduni na Elimu

Mradi wa pamoja wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO, la idadi ya watu na afya ya uzazi, UNFPA na lile linalohusika na masuala ya wanawake UN Women, uliotekekezwa katika wilaya nne za Tanzania ambazo ni Mkoani Pemba, Ngorongoro, Sengerema na Kasulu, matunda yake yameendelea kuonekana.

Huyo ni Jeska, mwanafunzi katika Shule ya Sekondari Kasulu iliyoko mkoani Kigoma, kaskazinimagharibi mwa Tanzania mmoja tu wa mfano wa manufaa ya mradi wa pamoja wa UNESCO, UNFPA na UN Women. Msichana huyu alipokuwa kidato cha tatu, alikuwa amekata tamaa ya kuendelea na masomo, 

Kupitia mradi huu wa Tuseme, Kilabu salama zaidi ya 110 zilitoa kwa wavulana na wasichana elimu ya kina ya ushauri kuhusu masuala ya uzazi, ujasiriamali kina kuhusu huduma ya ushauri wa ujinsia na nasaha  na ujuzi mwingine wa maisha. Jeska anaendelea kueleza alivyofaidika na mradi huu akisema,  

Selestino ni baba mzazi wa Jeska, mradi huu umempa furaha,  

Almachius Njugani ni Afisa anayesimamia mradi huu katika wilaya ya Kasulu,  

Aliyoyasema Afisa mradi yanathibitishwa na Afisa Elimu wa Wilaya ya Kasulu, Bwana Bahati Ernest Onesmo 

 Kwa mujibu wa UNESCO, asilimia 40 ya wasichana balehe nchini Tanzania wanaacha shule kutokana na changamoto mbalimbali zikiwemo ndoa za mapema, ujazuzito, umaskini na unyanyasaji wa kijinsia.