Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Angelina Jolie awasili Yemen kukutana na walioathiriwa na migogoro

Angelina Jolie, Mjumbe Maalum wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), akihutubia mkutano wa Mawaziri wa Kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 2019 katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.
UN Photo/Cia Pak

Msaada wa Kibinadamu

Mjumbe Maalum wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, Angelina Jolie amewasili Yemen leo kwa ziara ya kusaidia kuonesha athari mbaya za mzozo wa miaka 7 kwa watu wa Yemen. 

Angelina Jolie atakuwa akitembelea familia za watu wa Yemen, ikiwa ni pamoja na familia zilizofurushwa na pia wakimbizi ili kusikia moja kwa moja kutoka kwao jinsi mzozo huo ulivyosambaratisha maisha yao. 

UNHCR inatumai kuwa ziara yake itaangazia ongezeko la mahitaji ya kibinadamu nchini Yemen na kusaidia kuhamasisha uungaji mkono wa dharura kwa kazi ya kibinadamu nchini Yemen kabla ya Mkutano wa ngazi ya juu wa  kila mwaka wa Ahadi kwa ajili ya Yemen tarehe 16 Machi na kutoa wito kwa wahusika wa kikanda na kimataifa kujitolea kukomesha mzozo.