Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutozingatia masharti ya matumizi ya viuavijiumbe maradhi ndio chachu ya usugu wa dawa:FAO

Mazingira safi katika maeneo ya mifugo inaweza kupunguza matumizi ya viuavijasumu
FAO/Sergei Gapon
Mazingira safi katika maeneo ya mifugo inaweza kupunguza matumizi ya viuavijasumu

Kutozingatia masharti ya matumizi ya viuavijiumbe maradhi ndio chachu ya usugu wa dawa:FAO

Afya

Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limesema ongezeko la usugu wa viuavijiumbe maradhi yaani dawa zinazopambana na vimelea vya maradhi unatokana kwa kiasi kikubwa na kutozingatia marshi ya matumizi ya dawa hizo hususani katika kilimo na ufugaji. 

Wakati wiki ya kukuza uelewa kuhusu viuavijiumbe maradjhi ikieelekea ukingoni Dkt Elibariki Reuben Mwakapeje, afisa wa FAO nchini Tanzania anayeratibu udhibiti wa usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa, amesema hilo ni tatizo ambalo linasababisha madhara makubwa kwa ulimwengu kama tafiti za shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO linavyoeleza. 

Takwimu hizo zinasema kuwa usugu wa dawa unasababisha vifo 700,000 kila mwaka na huenda vitafikia vifo milioni mbili na zaidi ifikapo mwaka 2030. 

Akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa Dkt. Elibariki amesema Usugu wad awa “ Ni ile hali inayojitokeza kwamba dawa mbalimbali ambazo awali zilikuwa zikitibu magonjwa kwa binadamu na kwa wanyama awali sasa hivi dawa hizohizo hazifanyi kazi tena kutibu magonjwa hayo”. 

Je nini kinachangia hilo? 

Dkt. Elibariki anasema kuna sababu kuu mbili “Sababu ya kwanza ni kwamba vimelewa vya magonjwa vinajibadilisha viini tete vyake au DNA, na kujijengea hali ya kujikinga na mazingira mbalimbali na kwa kufanya hivyo inafanya iweze kukabiliana na ukali wa dawa inapotumika katika kutibu.” 

Sababu ya pili amesema “ Ni pale ambapo tunakula mazao ya mifugo au ya kilimo ambapo dawa zinakuwa zimetumika katika maeneo hayo mara kwa mara hata kwa kiwango kidogo. Mfano mifugo mbuzi au kuku akipewa dawa kutibu ugonjwa kunakuwa na kipindi cha mpito ambapo mazao ya mifugo hiyo inapaswa yasitumike kwa siku tatu au nne au tano lakini shida inayojitokeza ni kwamba utaratibu huu hauzingatiwi, utashangaa mfugo kama ng’ombe amepigwa dawa au ametibiwa leo na jioni unakamua maziwa unayatumia au kuku amepewa dawa , mayayi yake yanakuwa tayari yana dawa hizo, hivyo binadamu tunavyotumia  mazao ya mifugo hiyo ndivyo ambavyo tunakula hizo dawa kwa dozi kidogokidogo na wakati tunapougua na kwendfa hospitali dawa tunazopewa ndipo zinaposhindwa kutibu maradhi kwani zimeshakuwa sugu mwilini.” 

Na kwa upande wa kilimo na mazao yake inakuwaje? 

Kwa mujibu wa Dkt. Elibariki nisawa kama ilivyo kwenye mifugo “Na wenyewe unapita katika mfumo huohuo, tuna dawa nyingi sana tunazotumia dhidi ya wadudu wadhurifu mashambani, mfno mtu anapuliza dawa asubuhi kwenye bustan ya nyanya na jioni anachuma anapeleka sokoni au nyumbani kutumia kwa kufanya hivyo tunakula na zile kemikali ambazo ziko kwenye mazao. Kwa kufanya hivyo mfululizo ndivyo ambavyo sekta ya kilimo inachangia kuwepo kwa usugu wa dawa dhidi ya vimelea vya magonjwa.” 

Mbali ya hayo Dkt. Elibariki ameongeza kuwa kwa mifugo hata “Kinyesi chao baada ya kutumia dawa hizo yatari kinakuwa na kiasi kikubwa cha kemikali hivyo ukichukua hiyo mbolea na kutumia shambani sumu hiyo itatoka kwenye kinyeshi kwenda kwenye mmea na hadi kwenye mazao na ndipo FAO inayoshesha kwamba ushirikiano baina ya shughuli za kilimo unachangia uwepo wa vimelea hivyo.”

Mkazi huyu wa Ha Nam nchini Vietnam mwenye umri wa miaka 68 akionesha dawa zake za kutibu ugonjwa wa kisukari
© WHO/Quinn Mattingly
Mkazi huyu wa Ha Nam nchini Vietnam mwenye umri wa miaka 68 akionesha dawa zake za kutibu ugonjwa wa kisukari
Kwa kulitambua hilo FAO inachukua hatua gani?  

Dkt. Elibariki anasema “Tunafanya tafiti za kujua mabadiliko ya tabia kwa mfano tunaona maeneo mengi ya wafugaji wengi wanatumia dawa bila kufuata utaratibu wa wataalam , mfugaji mwenyewe anaenda duka la dawa ananunua na aenda kumdunga au kumtibu myanma nay eye sio mtaalam kwa kufanya hivyo anaweza kutoa kiwango cha dawa ambacho si sahihi kulingana na ugonjwa wenyewe au badala ya dawa za kumeza au maji anadunga sindano hayo ni matumizi holela ya dawa.” 

Na ameongeza kuwa ili kuepuka hilo baada ya kuzibaini tabia hizo wanatoa elimu kwa wafugaji kuhusu masuala ya msingi “Utoe chanjo kiwa mifugo yako ili wasiugue sababu wasipougua hawalazimika kutumia dawa, lakini pia mifugo ikiumwa uwe na utaratibu wa kutafuta wataalam wa mifugo, na ukipewa ushauri wa kitaalm uzigatie na dawa itumike kama inavyotakiwa ili tatizo liweze kupungua.”