Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres:Tubadili mwelekeo au mkutano wa mabadiliko ya tabianchi hautafanikiwa

Kusini mwa nchi ya Mauritania, shamba la mboga za majani linalomilikiwa na chama cha ushirika cha wanawake linatumia umeme wa jua kumwagilia mazao
© UNICEF/Raphael Pouget
Kusini mwa nchi ya Mauritania, shamba la mboga za majani linalomilikiwa na chama cha ushirika cha wanawake linatumia umeme wa jua kumwagilia mazao

Guterres:Tubadili mwelekeo au mkutano wa mabadiliko ya tabianchi hautafanikiwa

Tabianchi na mazingira

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa mshikamano na hatua madhubuti ili kuepusha janga la mabadiliko ya tabianchi

Guterres ametoa wito huo wakati akizungumza kwenye majadiliano yasiyo rasmi yaliyojikita katika suala la mabadiliko ya tabianchi. 

Amewaomba viongozi wanaohudhuria mkutano huo "kufanya kile kinachohitajika ili mkutano wa mabadiliko ya tabianchi COP26 ufanikiwe na kuwa alama ya mwanzo wa mabadiliko.” 

Katika tukio hilo lililofanyika leo Septemba 17 , 2021 kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani Katibu Mkuu ametuma ujumbe wa dharura kwa kikundi kidogo cha wakuu wa nchi na serikali waliokutanika kabla ya kuanza kwa mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya tabianchi wa 2021 (COP26) uliopangwa kufanyika Novemba akisisitiza kwamba “Endapo hatubadiliki kwa pamoja basi kuna hatari kubwa ya kutofaulu." 

Msisitizo mkubwa wa António Guterres unakuja baada ya kuchapishwa Ijumaa iliyopita ya ripoti ya mkataba wa mfumo wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya tabianchi UNFCCC ambao unajumuisha michango na ahadi zlizowekwa kitaifa na nchi, ya hatua madhubuti za kupunguza athari za ongezeko la joto duniani. 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, michango hii iko mbali na lengo la kudhibiti na ongezeko la joto la wastani duniani ili kuhakikisha linasalia nyuzi joto 1.5, kama ilivyokubaliwa na jamii ya kimataifa katika Mkataba wa Paris. 

"Kulingana na ahadi za sasa za nchi wanachama, ulimwengu uko katika njia mbaya kuelekea nyuzitojo 2.7 C.” 
Sayansi inatuambia kwamba kuzidi nyuzi joto1.5 itakuwa janga, "ameonya Guterres katika majadiliano hayo yaliyoitishwa kwa pamoja na mkuu wa Umoja wa Mastaifa na waziri mkuu wa Uingereza, Boris Johnson. 

Guterres amesisitiza kuwa, kudhibiti ongezeko la joto ili kusalia katika nyuzi joto 1.5, ni lazima kupunguzwa kwa uzalishaji wa hewa chafuzi kwa asilimia 45 ni ifikapo mwaka 2030, ambao utasaidia kufikia lengo la kutokomeza kabisa uzalishaji wa hewa ukaa katikati ya karne. 

"Kinyume chake, ahadi zilizotolewa na nchi hadi sasa zinamaanisha kutakuwa na ongezeko la asilimia 16% ya uzalishaji wa gesi chafu ifikapo mwaka 2030 ikilinganishwa na viwango vya 2010. Hii inamaanisha tusipochukua hatua tukibadilisha mwendo kwa pamoja, kuna hatari kubwa kwamba COP26 itashindwa kufanikiwa” ameongeza. 

Baianoai zilizopo baharini zinatoa chakula, maisha na usalama kwa zaidi ya watu bilioni duniani
Ocean Image Bank/Matt Curnock
Baianoai zilizopo baharini zinatoa chakula, maisha na usalama kwa zaidi ya watu bilioni duniani

 

Kuna mianya mitatu kabla ya mkutano wa COP26 

Ili kufanikisha hili, Guterres ametaja masuala matatu ya msingi: 
• kudumisha lengo la kutozidi nyuzi toto1.5C ya Mkataba wa Paris, 
• kutimiza ahadi iliyotolewa na nchi zilizoendelea ya kuchangia dola bilioni 100 kila mwaka kwa hatua za mabadiliko ya tabianchi katika nchi zinazoendelea 
• kuongeza uwekezaji wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa angalau asilimia 50% ya fedha za jumla za ufadhili wa umma wa mabadiliko ya tabianchi. 

Wakati huo huo kwa suala la upunguzaji kiwango cha joto, amesisitiza kwamba lengo la kudhibiti nyuzi joto kusalia 1.5C bado linawezekana kulingana na takwimu  zilizotolewa na kikundi cha wataalam wa kutoka nchi mbalimbali kuhusu mabadiliko ya tabianchi, lakini hiyo ni mabadiliko makubwa ya michango iliyowekwa kitaifa kutoka nchi nyingi. 

“Ninaelewa kanuni ya majukumu ya pamoja lakini yaliyotofautishwa. Nchi zilizoendelea lazima zichukue hatua. Lakini ni muhimu pia kwamba nchi za uchumi unaoibuka ziende hatua moja zaidi na kuchangia vyema kupunguza uzalishaji wa hewa chafuzi. Tunahitaji haswa uongozi wa nchi za G20.” Amesisitiza na kukumbusha kuwa mataifa haya yanachangia asilimia 80 ya uzalishaji wa gesi chafu. 

Uchafuzi wa hewa kutoka kwenye viwanda vinavyotumia makaa ya mawe unahusika kwenye kuongeza joto la dunia na matatizo mengine ya kimazingira na afya ya umma
Unsplash/Kouji Tsuru
Uchafuzi wa hewa kutoka kwenye viwanda vinavyotumia makaa ya mawe unahusika kwenye kuongeza joto la dunia na matatizo mengine ya kimazingira na afya ya umma


 Vita dhidi ya makaa ya mawe 

Guterres amesisitiza tena wito wake kwa serikali kuondoa ruzuku ya mafuta kisukuku na kumaliza matumizi ya makaa ya mawe.  
Kwa mfano, amesema kwamba ikiwa mitambo yote ya umeme inayopangwa kwa makaa ya mawe itaanza kufanya kazi, ongezeko la joto juu ya nyuzi joto 2C litazidi. 
“Malengo ya Paris yatatoweka. Nchi za OECD (Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo) lazima zimalize matumizi ya makaa ya mawe ifikapo mwaka 2030. Nchi zinazoendelea lazima zifanye hivyo mwaka 2040”, ameongeza. 
Guterres pia ameeleza kama ni"kutofaulu" fedha ambazo nchi zilitoa kwa mataifa yanayoendelea wakati wa 2019 na 2020 na akasihi kundi la mataifa ya ulimwengu wa kwanza kupunguza pengo hili. 
Vivyo hivyo, aliomba msaada wa taasisi za kifedha za kimataifa na uhamasishaji wa sekta binafsi kupitia msaada wa kifedha na teknolojia.