Skip to main content

Mwaka 2020 ni miongoni mwa miaka mitatu yenye joto zaidi kuwahi kurekodiwa-WMO

Jua likichomiza kutoka umbali wa mita 5000 nyuma ya mlima Iztaccihualt nchini Mexico
Picha na WMO/Miguel Angel Trejo Rangel
Jua likichomiza kutoka umbali wa mita 5000 nyuma ya mlima Iztaccihualt nchini Mexico

Mwaka 2020 ni miongoni mwa miaka mitatu yenye joto zaidi kuwahi kurekodiwa-WMO

Tabianchi na mazingira

Mwaka 2020 ulikuwa ni miongoni mwa miaka mitatu yenye joto zaidi kuwahi kurekodiwa huku ukichukua nafasi ya tatu baada ya mwaka 2016 kwa mujibu wa takwimu kupitia vipimo tano tofauti za shirika la Umoja wa utabiri wa hali ya hewa WMO. 

Kwa mujibu wa ripoti kuhusu utafiti wa WMO, vipimo tano tofauti vinaashiria kwamba muonfo 2011-2020 ulikuwa wenye joto zaidi kuwahi kurekodiwa katika mwenedo wa muda mrefu wa mabadiliko ya tabianchi. Miaka sita yeney joto zaidi imekuwa tangu 2015 huku miaka ya 2016, 2019 na 2020 ikichukua nafasi za tatu za kwanza huku tofauti ya viwango vya joto ikiwa ni ndogo. 

Wastani wa nyuzi joto kimatifa mwaka 2020 ilikuwa ni 14.9 katika kipimo cha Selsiyasi ikiwa ni 1.2 juu ya viwango vya kabla ya ukuaji wa viwanda miaka ya 1850-1900. 

Akizungumzia ripoti hiyo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema, “uthibitisho wa mwaka 2020 na WMO kama moja wa miaka yenye joto zaidi kuwahi kurekodiwa ni kumbusho la kazi ya mabadiliko ya tabianchi na ambavyo inaathiri maisha na vyanzo vya maisha katika sayari dunia. Leo tuko katika nyuzi joto 1.2 na tayari tunashuhudia mabadiliko yasiyotabirika ya hali ya hewa katika kila ukanda na bara. Tunaelekea katika viwango hatari vya kupanda kwa nyuzi joto 3 hadi 5 kwa kipimo cha Selsiyasi katika karne hii. Kufanya amani na mazingira ni moja ya jukumu letu karne hii ya 21. Ni lazima iwe kipaumble ya kila mmoja wetu kila mahali.” 

Kwa upande wake katibu mtendaji wa WMO, Profesa Petteri Taalas amesema, “viwango vya juu vya joto mwaka 2020 vilikuwepo licha ya kuwepo kwa La Niña ambayo huleta baridi kidogo. Ni jambo la kushangaza kwamba nyuzi joto mwaka 2020 zilikwenda sambamba na viwango mwaka 2016, wakati tulishuhudia moja ya matukio makubwa ya El Niño ambayo huchangia joto. Huu ni ushahidi tosha kwamba vihocheo vitokanavyo na shughuli za binadamu zina nguvu sawia na nguvu za asili.” 

 Profesa Taalas ameongeza kwamba viwango vya joto vya kila mwaka vinaashiria taswira kubwa zaidi na kwamba tangu miaka ya 1980 kila muongo umekuwa na nyuzi joto zaidi kuliko muongo uliontangulia.  

  La Niña iliyoanza mwishoni mwa mwaka 2020 inatarajiwa kuendelea hadi mapema au katikati ya mwaka 2021. Athari za La Niña na huwa kali zaidi mwka wa pili baada ya matukio hayo. 

Joto Kali na mioto ya nyikani huko Siberia na kupungua kwa barafu kwenye bahari ya Arctic pamoja na vimbunga kwenye Atlantiki vilikuwa miongoni mwa matukio makubwa ya mkwa 2020. 

Kama ilivyo katika miaka ya awali kulikuwa na athari kubwa za kiuchumi na kijamii mwaka 2020, kwa mfano mwaka majanga yaliigharimu Marekani dola bilioni 22 mwaka 2020, ukiwa ni mwaka wa tano kwa viwango vya joto kuwahi kurekodiwa.