Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni lazima tuchague amani na si zahma kuinusuru dunia:Guterres

Watoto wakiwa katika kituo cha kulelea watoto yatima nchini Suda Kusini, wakirekodi wimbo wa amani ambao ulichezwa kwenye redio zote nchi nzima
UNMISS/Gregório Cunha
Watoto wakiwa katika kituo cha kulelea watoto yatima nchini Suda Kusini, wakirekodi wimbo wa amani ambao ulichezwa kwenye redio zote nchi nzima

Ni lazima tuchague amani na si zahma kuinusuru dunia:Guterres

Amani na Usalama

Katika kuelekeaa siku ya amani duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka Septemba 21, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameiasa dunia lazima kuchagua Amani au hatari ya kudumu akisema janga la COVID-19 limepindua maisha ya watu huku vita vikitapakaa kila kona na kwa kiwango cha kupindukia. 

Amesema pia "Dharura ya mabadiliko ya tabianchi inazidi kuwa mbaya huku pengo la kutokuwepo kwa usawa linapanuka na umasikini umefurutu ada, na suala la kutoaminiana na migawanyiko kunawashinikiza watu katika wakati ambao mshikamano na ushirikiano unahitajika kuliko wakati Mwingine wowote." 

Kwa mantiki hiyo Katibu Mkuu  ametoa wito wa kusitisha uhasama kwa 24 akisistiza kuwa “Kama familia ya kibinadamu tunakabiliwa na uchaguzi muhimu, wa amani au machungu ya muda mrefu. Ni lazima tuchague amani leo na kufanya kazi kwa mshikamano kwa ajili ya kufikia amani ya kudumu, na endelevu kila siku na tunaweza kushughulikia kwa pamoja changamoto zinazotukabili.” 

Amesisitiza kwamba “Tunahitaji amani haraka ili kupeleka chanjo za kuokoa maisha dhidi ya coronavirus">COVID-19. Tunahitaji amani ili kujikwamua vyema kutoka kwenye janga hilo, kujinga upya mifumo iliyosambaratika na maisha ya mamilioni ya watu yaliyoathirika.” 

Pia ameongeza kuwa tunahitaji amani kuwema mambo katika msitari na kupunguza pengo la usawa, kurejesha Imani miongoni mwa watu, katika imani na katika sayansi na pia tunahitaji kuwa na amani na mazingira, kuiponya sayari yetu, kujenga uchumi unaozingatia mazingira na kutimiza lengo la kutokomeza kabisa hewa ukaa. 

Kwani amekumbusha kwamba amani sio ndoto bali ni mwanga gizani unaoiongoza dunia katika njia pekee ya mustakbali bora kwa binadamu wote. 

Guterres amehitimisha kwa wito maalum kwamba “Hebu na tufuate njia ya amani kama vile maisha yetu hayawezi kuwepo bila hiyo, kwani huo ndio ukweli halisi.”