Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usitishaji uhasama kimataifa, kusaidia wasiojiweza na mikakati ya kujikwamua ndio kipaumbele cha UN:Guterres

Katibu Mkuu Antonio Guterres akitoa ujumbe kuhusu Janga la COVID-19.
UN Photo/Eskinder Debebe)
Katibu Mkuu Antonio Guterres akitoa ujumbe kuhusu Janga la COVID-19.

Usitishaji uhasama kimataifa, kusaidia wasiojiweza na mikakati ya kujikwamua ndio kipaumbele cha UN:Guterres

Amani na Usalama

 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo Alhamisi ameweka bayana dhimira ya Umoja wa Mataifa ya kutaka kuvishinda vita dhidi ya janga la virusi vya corona au COVID-19  kwa kujikita na mambo matatu muhimu ambayo ni kufikia usitishwaji wa uhasama kimataifa, kuwasaidia wale wasiojiweza na kujiandaa kujikwamua kiuchumi na kijamii kutoka kwenye janga hili.

 Katika mkutano na waandishi wa Habari kuputia mtandao Guterres ameelezea hofu yake “kuhusu kuhusu kutokuwepo kwa mshikamano wa kutosha nan chi zinazoendelea  kwa kuziwezesha kupambana na janga la COVID-19 ambalo linauwezekano wa kusambaa kama moto wa nyika na kukabiliana na athari za kiuchumi na kijamii.”

Amesisitiza uhamasishaji wa mfumo mzima wa Umoja wa Mataifa , mashinani na makao makuu mjini New York kuzuia njaa na kufanya mipango ya kujikwamua.

Amegusia ndege za mshikamano ambazo zimewezesha kusafirishwa kwa vifaa karibu tani 1200 vya kupima wagonjwa na vifaa vingine vya kitatibu kwa karibu nchi 52 za Afrika.

Mambo makuu matatu ya kutimza

Katibu Mkuu ametangaza hatua kuu tatu za juhudi za Umoja wa Mataifa kujikwamua kutoka kwenye janga hili la COVID-19

Kipaumbele cha kwanza amesema ni kufikia usitishwaji mapigano wa kimataifa . Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema wito wake wa kusitisha uhasama umepokea mwitikio mkubwa kwa msaada wa serikali 114, mashirika ya kikanda, viongozi wa kidini na zaidi ya makundi 200 ya asasi za kiraia katika kanda zote na miongoni mwao vikundi 16 vya wapiganaji.

“Lakini tunajua kwamba kutoaminiana bado kuko juu n ani vugumu kuendelea na utekelezaji” amesema Guterres  na kuongeza kuwa wajumbe na wawakilishi wake maalum wamefanyakazi bila kuchoka na wakati mwingine kuwa katika hatari ili kubadili maazimio hayo kuwa vitendo vya usitishaji uhasama.

Katibu Mkuu amegundua na kubaini kwamba amebaini na kuridhika kwamba nchini Syria usitishwaji mapigano katika jimbo la Idlib unaheshimiwa, hata hivyo bado ana matumaini kwamba usitishaji uhasama huo utakamilika nchini kote.

Nchini Yemen anahisi bado kuna uwezekano wa amani. Huko Libya kwa upande mwingine amesema “Tunashuhudia kuongezeka kwa machafuko licha ya juhudi zetu zote na za wengine wengi katika jumuiya ya kimataifa.”

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu juhudi zote hizi zinategemea uungaji mkono imara wa kisiasa na anatumai kwamba Baraza la Usalama litapitisha maamuzi ambayo yatasaida kufanya usitishwaji uhasama kuwa wa maana na wa kweli.

Katibu Mkuu Antonio Guterres akihutubia  waandishi wahabari kutumia njia  ya Video.
UN Photo/Eskinder Debebe)
Katibu Mkuu Antonio Guterres akihutubia waandishi wahabari kutumia njia ya Video.

 

Msaada mkubwa wahitajika kwa nchi zinazoendelea

Kipaumbele cha pili cha Umoja wa Mataifa Bwana Guterres amesema ni kuendelea kukidhi mahitajo ya sasa kwa wale wanaokabiliwa na changamoto kubwa ya kiuchumi. “Nitaendelea kuchagiza kuwa na mipango ya usaidizi ya asilimia kubwa ya uchumi wa dunia angalau asilimia 10 . Nchi nyingi zilizoendelea zinaweza kujikimu kwa rasilimali zake, lakini nchi zinazoendelea zinahitaji msaada mkubwa na wa haraka.”

Na kipaumbele cha tatu ni kuanza mipango ya kujikwamua kutoka kwenye janga hili sasa. “Kujikwamua kutoka kwa janga la COVID-19 kunaweza kusaidia dunia kuwa salama, yenye afya , endelevu Zaidi na ya njia jumuishi.Ni muhimu kukabiliana na mapengo ya usawa katika hifadhi ya jamii ambayo yamekuwa na machungu makubwa na kuwaweka wanawake na usawa wa kijinsia katika kitovu cha hofu zetu kama tunataka kujenga mnepo baada ya janga hili.”

Mwisho amehimiza kwamba “Kujikwamua lazima kuende sanjari na hatua za mabadiliko ya tabianchi” Na kwa mantiki hiyo ametoa wito kwa serikali kuhakikisha kwamba matumuzi ya kufufua uchumi ynasongesha pia juhudu za kupunguza hewa ukaa katika Nyanja zote za uchumi na kutoa kipaumbele katika ajira zinazojali mazingira.