Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miaka 10 ya vita Syria jinamizi bado liko palepale:UN 

Muongo wa vita Syria umewabebesha ghara kubwa wanawake na wasichana
© UNFPA Syria
Muongo wa vita Syria umewabebesha ghara kubwa wanawake na wasichana

Miaka 10 ya vita Syria jinamizi bado liko palepale:UN 

Amani na Usalama

Wakati vita vya Syria vimetimiza muongo mmoja ulioghubikwa na madhila ya hali ya juu, mjumbe maalum wa Umoja wa Matyaifa nchini humo ameliambia Baraza la Usalama leo Jumatatu kwamba "Vita hivyo vitaingia katika historia kama vita vya vibaya zaidi na vilivyoghubikwa na kiza kikuu katika miaka ya hivi karibuniya hivi karibuni akimaanisha kwamba watu wa Syria kama waathirika wakubwa wa karne hii . 

"Ninataka kuwakumbuka waathirika wa Syria na kukumbuka mateso ya Syria na mnepo wao katika machafuko yasiyo na kifani na madhila ambayo wamekutana nazo kwa zaidi ya miaka kumi", amesema Mjumbe huyo maalum Geir Pedersen akisoma litani ya ukiukaji uliofurutu ada wa sheria za kimataifa, pamoja na jinamizi baya la silaha za kemikali. 

Geir O. Pedersen, mjumbe maalum wa Katibu Mkuu kwa ajili ya Syria akitoa taarifa kwa njia ya mtandao kwenye Baraza la Usalama wakato wa kikao cha wazi kuhusu hali ya Syria
UN Photo/Loey Felipe
Geir O. Pedersen, mjumbe maalum wa Katibu Mkuu kwa ajili ya Syria akitoa taarifa kwa njia ya mtandao kwenye Baraza la Usalama wakato wa kikao cha wazi kuhusu hali ya Syria

Taswira ya kutisha 

Mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa amesema Waasyria "wamejeruhiwa, wamelemazwa na kuuawa kwa kila njia inayowezekana maiti zao hata zimetiwa unajisi na wengine kutupwa katika magereza au kutekwa nyara, kuteswa, kupangwa katika mazizi na kuwekwa rehani kwa ajili yya kikombozi". 

Pia ametanabaisha “hali halisi ya Wasyria waliotawanywa tena na tena wakilazimishwa kulala nje katika iwe ni kwenye joto kali na hata kunapomiminika theluji, kwani nyumba, hospitali na shule zimeharibiwa na mashambulio ya anga, mabomu na moto wa roketi.” 

Ameongeza kuwa raia "Wamekuwa wakinyimwa usaidizi wa kibinadamu, wakati wakiwa wamezingirwa ambapo wahusika wanaowazingira wakiwalaza njaa kwa makusudi, watu hao wanakabiliwa na ukiukaji wa haki za binadamu kwa kiwango kikubwa kisicho na mfano. 

"Wanawake wa Syria wamekabiliwa na unyanyasaji wa kingono kutoka pande zote na kuongezeka kwa ndoa za utotoni na za kulazimishwa", ameongeza. 

Wakati huo huo, Bwana Pederson  amesema “raia wanalazimika kukabiliana na janga la COVID-19 na mfumo wa afyaulio na mapungufu na uliosambaratika, ameendelea kusema mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa, akibainisha kuwa watoto wengi hawajawahi kuishi siku bila vita na wengi wamekosa chakula, dawa au elimu , au kuzuiliwa, kuajiriwa kwenye vita, kujeruhiwa au kuuawa ”. 

Mhudumu wa afya akizungumza na watoto wakimbizi kuhusu matumaini na hofu zao kwenye kambi ya Atma nchini Syria.
© UNOCHA/Mahmoud Al-Basha
Mhudumu wa afya akizungumza na watoto wakimbizi kuhusu matumaini na hofu zao kwenye kambi ya Atma nchini Syria.

Maisha yaliyoghubikwa na jinamizi 

Kwa muongo mmoja uliopita, Wasyria hawajaona maelewano yote kati ya maono kinzani ya kisiasa, au maendeleo yoyote ya kweli katika mazungumzo kati ya serikali na upande wa upinzani ili kuweza kupatanishwa, kulingana na Bwana Pedersen 

Kwa kuongezea, amesema wale wanaohusika na vitendo ambavyo vinaweza kuwa uhalifu dhidi ya ubinadamu au uhalifu wa kivit wanafurahia kukwepa sheria, hali ambayo sio tu inadhoofisha makubaliano ya amani lakini jinamizi ambalo limekuwa ndio maisha nchini Syria. 

"Wasyria wote wameona kuwa jamii ya kimataifa imegawanyika, imenaswa katika mashindano ya kijiografia, imeshikwa katika hadithi zao zenye kushindana, na mara nyingi imejikita katika kuunga mkono upande mmoja au mwingine katika vita." 

Ulimwengu haujafanikiwa kusaidia kuleta amani kwa raia wa kawaida, amesema, akisisitiza haja ya kutafuta njia ya kuzunguka ugonjwa wa "wewe kwanza" ambao unaashiria diplomasia ya hapo. 

"Hivi sasa, kuna madai kuna kwa pande zote lakini harakati ni kidogo kwa kila ", ameonya. 

Tarehe 19 Januari mwaka 2021,watoto wakiwa nje ya mahema yaliyozingirwa na maji kwenye kambi ya Kafr Losin Kaskazini-Magharibi mwa Syria.
© UNICEF/Khaled Akacha
Tarehe 19 Januari mwaka 2021,watoto wakiwa nje ya mahema yaliyozingirwa na maji kwenye kambi ya Kafr Losin Kaskazini-Magharibi mwa Syria.

Suluhisho la kisiasa ndio njia pekee 

Ili kusonga mbele, mjumbe wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kwamba Serikali ya Syria, upinzani na wadau muhimu wa kimataifa lazima watambue sio tu kile wanachotarajia kufikia, lakini jinsi wanavyoweza kusongesha azimio namba 2254, ambalo linataka kusitisha mapigano na suluhu ya kisiasa nchini humo. 

"Wakati ambapo kuna changamoto nyingi kubwa, tusipoteze mwelekeo wa kimsingi wa utatuzi wa amani wa mzozo wa Syria", amesema. "Suluhisho la kisiasa ndiyo njia pekee ya kutoka kwenye zahma hiyo na ninauhakika kuwa inawezekana".