Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waliokufa na kipindupindu nchini Nigeria wafikia 45

Watoto kutoka katika familia zilizoparaganyika katika eneo la Maiduguri, jimboni Borno, kaskazini mashariki mwa Nigeria wakikinga maji. Mgogoro katika eneo hilo umewalazimisha mamia ya maelfu kuyahama makazi yao na kuishi kwa kutegemea misaada.
UNICEF/Gilbertson VII Photo

Afya

Watu watatu wamekufa katika jimbo la Borno nchini Nigeria kutokana na kuugua kipindupindu na hivyo kufanya jumla ya vifo nchini humo kufikia 45. 

Taarifa ya pamoja iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO Pamoja na Wizara ya afya ya Borno imeeleza kuna maambukizi mapya 69 ya wagonjwa wa kipindupindu yamefanya idadi ya wagonjwa kufikia 666 jimboni humo. 

Juhudi mbalimbali za kukabiliana na ugonjwa huo zinafanyika ikiwemo wataalamu wa afya kutembea maeneo yaliyoathirka zaidi ambapo wataalamu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto UNICEF wanashirkiana na WHO wanatembelea nyumba kwa nyumba hususan maeneo yaliyo hatarini zaidi. 

WHO inaendesha pia kampeni katika kambi za wakimbizi wa ndani na jamii zinazowahifadhi wakimbizi na maeneo yaliyo na idadi kubwa ya watu kupitisha ujumbe wa kuzuia kipindupindu pamoja na COVID-9 kwa watu zaidi ya 65, 000 jimboni kote.