Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya watu bilioni 4 bado wanakosa ulinzi wa hifadhi ya jamii

Mwanamke akiwa amembeba mtoto huku akiomba katika mitaa ya Chisinau huko Moldova.
ILO/Marcel Crozet
Mwanamke akiwa amembeba mtoto huku akiomba katika mitaa ya Chisinau huko Moldova.

Zaidi ya watu bilioni 4 bado wanakosa ulinzi wa hifadhi ya jamii

Haki za binadamu

Licha ya kuongezeka wigo wa hifadhi ya jamii ulimwenguni wakati wa janga la corona au COVID-19, zaidi ya watu bilioni 4 duniani kotebado hawana kabisa  ulinzi wa hifadhi ya jamii imesema ripoti mpya ya shirika la kazi la Umoja wa Mataifa ILO. 

Ripoti hiyo iliyotolewa leo inasisitiza kuwa hatua za kupambana na janga la COVID-19 hazikuwa za kutosha na zilikuwa za kutatanisha, zikipanua zaidi pengo kati ya nchi zenye kipato cha juu na kipato cha chini, na zimeshindwa kutoa ulinzi wa kijamii unaohitajika ambao kila mwanadamu anastahili. 

Ripoti inasema ulinzi wa jamii ni pamoja na upatikanaji wa huduma za afya na usalama wa kipato, haswa kwa wazee, na pia ikiwa kuna ukosefu wa ajira, magonjwa, ulemavu, ajali kazini, uzazi au kifo cha mlezi mkuu wa familia, na pia kwa familia zilizo na watoto.

Mkurugenzi mkuu wa ILO Guy Ryder katika ripoti hiyo amesema “Nchi ziko njiapanda. Huu ni wakati muhimu kutumia hatua za kupambana na janga hilo  na kujenga kizazi kipya cha mifumo ya haki za ulinzi wa jamii.” 

Kulingana na mkuu huyo wa ILO, kwa kulinda idadi kubwa ya watu kutokana na majanga ya siku za usoni, mifumo kama hiyo ya haki za hifadhi ya jamii ni muhimu kwani huwapa wafanyikazi na wafanyabiashara usalama wanaohitaji kukabiliana nayo kwa ujasiri na kutumaini mabadiliko mengi yanayowasubiri. 

"Lazima tutambue kuwa ulinzi kamili wa hifadhi ya kijamii na kwamba sio muhimu tu kwa haki ya kijamii na kazi nzuri, lakini pia husaidia kujenga mnepo endelevu na utulivu katika siku zijazo." ameongeza Guy Ryder  

Mfanyakazi wa kiwanda cha nguo akiwa kwenye chumba anakoishi na wengine saba katika mabweni ya kiwanda cha nguo nchini Jordan.
ILO/Marcel Crozet
Mfanyakazi wa kiwanda cha nguo akiwa kwenye chumba anakoishi na wengine saba katika mabweni ya kiwanda cha nguo nchini Jordan.

Kutafuta maisha bora ya baadaye 

Ripoti yakimataifa ya ulinzi wa hifadhi ya jamii 2020-22: “Ulinzi wa hifadhi ya Jamii ukiwa njia panda , kusaka mustakbali bora” hutoa muhtasari wa jumla wa maendeleo ya hivi karibuni katika mifumo ya hifadhi ya jamii, pamoja na majukwaa ya ulinzi wa jamii, na inashughulikia athari za janga la COVID-19. 

Ripoti hiyo inabainisha mapungufu ya hifadhi ya jamii na inatoa mapendekezo muhimu ya sera, pamoja na kuhusiana na malengo ya ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu. 

Hivi sasa, ni watu milioni 475 tu ya idadi ya watu ulimwenguni ndio ambao wanalindwa vyema na angalau faida moja ya mifumo ya hifadhi ya jamii, wakati watu bilioni 4.1  sawa na asilimia (53%) hawana uhakika wa kipato kupitia mfumo wao wa kitaifa wa hifadhi ya jamii. 

Kwa upande wa hifadhi ya jamii, pengo la usawa ni dhahiri. Ulaya na Asia ya Kati zina viwango vya juu zaidi vya chanjo, na asilimia 84 ya watu wao wanapokea angalau faida moja ya hudumua za hifadhi ya jamii.  

Amerika pia viwango viko juu ya wastani wa viwango vya dunia, ni asilimia 64.3%.  
Asia na Pasifiki ni asilimia (44%), huku Mataifa ya Kiarabu yakiwa katika asilimia (40%) na Afrika asilimia (17.4%) wana mapungufu ya wazi katika hifadhi ya jamii. 

Duniani kote, idadi kubwa ya watoto bado hawana ulinzi wa hifadhi ya jamii ni mmoja tu kati ya watoto wanne sawa na asilimia (26.4%) anayefaidika na ulinzi wa hifadhi ya jamii.  

Ni asilimia 45% tu ya wanawake walio na mtoto mchanga wanapewa posho ya uzazi.  
Ni mmoja tu kati ya walemavu watatu sawa na asilimia (33.5%) ulimwenguni hupokea malipo ya uzeeni ya watu wenye ulemavu.  
Malipo  ya ukosefu wa ajira ni ya chini zaidi: ni asilimia 18.6 tu ya wafanyikazi wasio na ajira ndio wamefunika na malipo hayo.  

Wakati asilimia 77.5% ya watu zaidi ya umri wa kustaafu wanapokea aina fulani ya malipo ya uzeeni, tofauti kubwa inaendelea kati ya nchi, kati ya miji na vijijini, na kati ya wanaume na wanawake. 

Matumizi ya umma kwa masuala ya hifadhi ya jamii pia yanatofautiana sana. Kwa wastani, nchi zinatumia asilimia 12.8 ya pato lao la jumla  la taifa kwa hifadhi ya jamii (bila masuala ya afya), hata hivyo nchi zenye kipato cha juu hutumia asilimia 16.4% ya pato la taifa na nchi zenye kipato cha chini ni asilimia 1, 1% tu. 

Mwanamke akiendesha kigari cha kunyanyua mizigo mizito katika kiwanda nchini Jordan
UNDP/Sumaya Agha
Mwanamke akiendesha kigari cha kunyanyua mizigo mizito katika kiwanda nchini Jordan

 Pengo la ufadhili 

Ripoti hiyo inasema kuwa katika pengo la ufadhili matumizi ya ziada yanahitajika ili kuhakikisha angalau ulinzi mdogo wa hifadhi ya jamii kwa wote kwani pengo  limeongezeka kwa karibu asilimia 30% tangu kuanza kwa janga la COVID-19. 

Ili kuhakikisha ulinzi wa msingi wa jamii, nchi zenye kipato cha chini zinapaswa kuwekeza nyongeza ya dola bilioni $ 77.9 kwa mwaka, nchi za kipato cha wastani wa chini zitaongeza dola bilioni $ 362.9 bilioni, na nchi za kipato cha kati  dola bilioni 750, ikiwa ni ongezeko la dola bilioni $ 8 zaidi kwa mwaka .  

Hii ni sawa, mtawaliwa, wa hadi asilimia 15.9%; 5.1% na 3.1% za pato la taifa. 
"Kuna shinikizo kubwa kwa nchi kuchagua ujumuishaji wa fedha, baada ya matumizi makubwa ya umma yanayohusiana na hatua zilizochukuliwa kushughulikia janga la COVID-19, lakini itakuwa mbaya sana kupunguza matumizi ya hifadhi ya jamii; wakati wa kuwekeza umefika na ni sasa” amesema Shahra Razavi, mkurugenzi wa idara ya ulinzi wa hjifadhi ya jamii ya ILO. 

Ameongeza kuwa “Ulinzi wa jamii ni zana muhimu inayoweza kuleta faida kubwa za kijamii na kiuchumi kwa nchi katika hatua zote za maendeleo. Unaweza kusaidia kuboresha afya na elimu kwa idadi ya watu, usawa zaidi, mifumo endelevu zaidi ya uchumi, usimamizi bora wa uhamiaji na kuheshimu haki za kimsingi za binadamu.” 

Hatua maalum za kukuza hifadhi ya jamii kwa wote ziliwekwa katika wito mpya wa kimataifa wa utekelezaji wa hatua za kujikwamua ambazo zinazingatia masuala ya kibinadamu kutoka kwenye janga hili la COVID-19. 

Wito huu wa hatua za kujikwamua na janga la COVID-19 ambazo zimeweka ajenda kamili ya kujikwamua, ulipitishwa kwa kauli moja mwezi Juni 2021 na nchi wanachama wa ILO, zikiwakilisha serikali, mashirika ya wafanyikazi na waajiri. 

"Ili kujenga mifumo inayoweza kutoa matokeo haya, lazima tuunganishe vyanzo vya fedha na kuimarisha mshikamano wa kimataifa, haswa kwa kusaidia nchi masikini," amesema Shahra Razavi. 

"Lakini gawio la mafanikio litapita mipaka ya kitaifa ili kufaidisha kila mtu,"