Kwa nini misaada ya kibinadamu hurushwa kutoka angani kwenye ndege? 

Ndege ya WFP ikisambaza chakula.
Maktaba/UN
Ndege ya WFP ikisambaza chakula.

Kwa nini misaada ya kibinadamu hurushwa kutoka angani kwenye ndege? 

Msaada wa Kibinadamu

Tukiangazia shughuli za usambazaji wa misaada ya kibinadamu, umewahi kujiuliza ni kwa nini wakati mwingine misaada ya kibinadamu husambazwa kwa njia ya gharama zaidi ya ndege kudondosha misaada hiyo kutoka angani? Afisa mmoja wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani, WFP anaeleza.

Kazi ya usambazaji wa misaada ya kibinadamu, wakati mwingine inawaweka njiapanda wasambazaji wa misaada hiyo pindi ambapo, wanaopaswa kusaidiwa wanapokuwa katika maeneo yasiyofikika kwa urahisi kwa usafiri wa kawaida. 

Kama anavyoeleza afisa huyu wa WFP, nyuma yake wanaonekana wafanyakazi wakikata mifuko ya sandarusi iliyojaa mtama ambao unakusudiwa kupelekwa katika eneo moja la Sudan Kusini ambalo kutokana na kuzungukwa na ardhi tepetepe ya bwawa, hapafifikiki kwa njia ya barabara. Na hata kwa njia ya helikopta, haiwezi kubeba mzigo wa kuwatosha watu walioko huko. 

(Nats) 

Afisa huyu anasema wafanyakazi hawa wanachofanya ni kukata gunia la juu na kumimina nafaka hizo katika mfuko mwingine na kisha kuweka mifuko mingine sita juu yake ili mzigo huu utakapodondoshwa kutoka kwenye ndege angani, mifuko au vigunia vya juu vinaweza kupasuka, lakini mfuko wa mwisho uliobeba chakula utabaki salama.  

Na sasa ndege kubwa ya mizigo ya WFP inapakia mzigo huo kisha inaiacha ardhi kuelekea Nyal, eneo lililozungukwa na linalotajwa kuwa bwawa kubwa zaidi ulimwenguni. 

Ndege hiyo baada ya kufika juu angani usawa wa eneo kame, huku chini ardhini yuko afisa mwingine ambaye anaielekeza kuwa sasa inaweza kuuachia mzigo udodondoke.  

Ndege inafungua mlango wake wa nyuma ikiwa katika kasi, tani 34 za magunia yaliyosheheni nafaka, zinadondoka kwa ajili ya watu 3000 kupata mlo angalau kwa mwezi mmoja.