Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kabla ya kukata msaada hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na magonjwa zichukuliwe:Lowcock

Mark Lowcok msaidizi wa Katibu Mkuu katika masuala ya kibinadamu na kuratibu misaada ya dharura akizungumza na baadhi ya wakimbizi wa ndani kwenye jimbo la Equatoria ya Katyi katika makazi ya Gezira nje kidogo ya mji wa Yei Sudan Kusini
UNMISS/Eric Kanalstein
Mark Lowcok msaidizi wa Katibu Mkuu katika masuala ya kibinadamu na kuratibu misaada ya dharura akizungumza na baadhi ya wakimbizi wa ndani kwenye jimbo la Equatoria ya Katyi katika makazi ya Gezira nje kidogo ya mji wa Yei Sudan Kusini

Kabla ya kukata msaada hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na magonjwa zichukuliwe:Lowcock

Msaada wa Kibinadamu

 Akitafakari miaka miine ya uongozi wake kama mratibu mkuu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa OCHA, Mark Lowcok amesema ni jinsi gani watu zaidi na zaidi wanavyohitaji msaada wa kibinadamu kwa sababu ya vita, mabadiliko ya tabianchi na magonjwa kama mlipuko wa Ebola na janga la corona au COVID-19.

Lowcock ambaye anaondoka mamlakani ni msaidizi wa Katibu mkuu kwa ajili ya masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura amezungumza na UN News kupitia ujuzi alionao ili kutanabaisha ni jinsi gani changamoto za dunia zinaweza kusgshughulikiwa .
Pia amesema ana matumaini makubwa hatsa kutokana na kazi inayofanywa na wahudumu wa kibinadamu ambao wamejitolea kusaidia wengine bila kuchoka.


Niliyotumai hayakuwa

Bwana Lowcock amersema alitumaini mambo yangeweza kubadili mkondo “Nilitarajia kuwa inawezekana kubadili mwenendo huo wa hivi karibuni kwa sababu katika zaidi ya miaka 50 iliyopita kumekuwa na maendeleo makubwa katika maendeleo ya binadamu, na watu wanaishi kwa muda mrefu, wamelishwa vizuri, watoto wengi wanaenda shuleni, wachache hufa na magonjwa yanayoweza kuepukika , Nakadhalika. Nilitumaini kwamba kiwango cha maendeleo hayo kingekuwa mara mbili na hivyo kupata njia ya kuwafikia watu walio hatarini zaidi ulimwenguni ambao kwa kawaida ni wale walio katika hali ngumu za kibinadamu. Lakini nadhani, kwa kusema wazi, miaka minne iliyopita imekuwa wakati mgumu zaidi.”
Ameongeza kuwa kwanza, tumekuwa na ongezeko la mizozo katika maeneo mengi, kushindwa kusuluhisha mizozo ya muda mrefu kama Syria na Yemen, na mizoz mipya kama Msumbiji, Ethiopia na kuongezeka kwa maeneo mengine.
Pili, tumeona kuongezeka kwa athari za mabadiliko ya tabianchi ambayo sasa ni sababu kubwa ya mateso ya kibinadamu ulimwenguni kote.
 Na tatu, tumekuwa na milipuko ya magonjwasio tu janga, lakini kwa kweli janga hilo limeleta tofauti kubwa.
“Kwa hivyo, ingawa lengo langu lilikuwa kuona kupunguzwa kwa mateso, kwa kweli kile kilichotokea ni ukuaji kwa viwango ambavyo havijawahi kutokea, kwa kweli, katika idadi ya watu ambao wanahitaji ulinzi na msaada wa kibinadamu.”

Mark Lowcock mkuu wa OCHA akihutubia Baraza la Usalama kuhusu hali nchini Yemen.
UN Photo/Manuel Elías
Mark Lowcock mkuu wa OCHA akihutubia Baraza la Usalama kuhusu hali nchini Yemen.


Bado kuna matumaini

Mratibu huyo mkuu amesema bado kuna matumaini kwani “habari njema ni kwamba Umoja wa Mataifa, NGOs, Chama cha Msalaba Mwekundu, na wadau wengine  wanaendelea kufanya kazi nzuri katika kuokoa maisha na kupunguza mateso, na nadhani mfumo wa kibinadamu umepiga hatua katika miaka ya hivi karibuni. Na tunawafikia watu zaidi ya milioni 100 kwa mwaka, tunaokoa mamilioni ya maisha kila mwaka, na mambo yatakuwa mabaya zaidi lakini kwa ujasiri na kujitolea na weledi wa kujitolea kwa watu wote wanaofanya kazi kwa mashirika ya kibinadamu ulimwenguni, ambao wengi wao, tukumbuke, ni raia, raia, wa nchi ambazo zina shida wenyewe.”

COVID-19 ni mwiba lakini OCHA imekuwa nguzo

Janga la COVIDF-19 amesema limeongeza madhila kwa mamilioni ya watu ambao tayari walikuwa katika dhidi na kutegemea msaada.
Hata hivyo amesema OCHA imekuwa msitari wa mbele kukabiliana na changamoto hizo kwa maslahi ya mamilioni ya watu hasa wakati wa janga la COVID-19.

Picha hii ya maktaba inamwonyesha Mkuu wa ofisi ya misaada ya dharura, OCHA, Mark Lowcock alipotembelea wahitaj wa chakula kwenye kitongoji cha Epworth, nje ya mji mkuu wa Zimbabwe, Harare mapema mwaka huu.
OCHA/Saviano Abreu
Picha hii ya maktaba inamwonyesha Mkuu wa ofisi ya misaada ya dharura, OCHA, Mark Lowcock alipotembelea wahitaj wa chakula kwenye kitongoji cha Epworth, nje ya mji mkuu wa Zimbabwe, Harare mapema mwaka huu.


“Kweli, kazi ya OCHA kimsingi ni kuwa mratibu wa mfumo wa misaada ya kibinadamu. Tulirekebisha jinsi tulivyojipanga. Tna watu wengi mashinani, wachache kwenye makao makuu. Tumeweka fedha zetu sawa. Nilipoanza kazi hii, OCHA ilikuwa inakabiliwa na shida nyingi za kifedha ambazo tumeweza kuzitatua. Na tumezingatia sana majukumu manne muhimu ambayo tunayo.”
 Bwana Lowcock ameyataja majukumu hayo kuwa ni pamoja na “Kwanza, kutambua hitaji la kibinadamu linapojitokeza. Pili, kuratibu ya mipango ya kukabiliana na mahitaji hayo katika kila nchi ambapo kuna shida. Tatu, kukusanya pesa kulipia mipango ya utekelezaji wa hatua hizo. Na kisha nne, kusaidia kwa maswala maalum juu ya utekelezaji,  kutokupeleka chakula au huduma ya matibabu au bidhaa kwa watu, lakini kusaidia kwa vitu kama mazungumzo ya ufikiaji wa amani katika mizozo na mifumo ya ukomeshaji mapigano ambapo wafanyikazi wa misaada ya kibinadamu wanahitaji kulindwa kutoka kwa wanaume wenye silaha na mabomu.”

Je! Umewahi kujuta kukubali kuchukua kazi hii ngumu?

Mark Lowcock akijibu swali hilo amesema “Kweli, unajua Katibu Mkuu alinipigia simu mnamo Aprili 2017 na kuniuliza ikiwa ningechukua kazi hiyo. Nadhani Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akikupigia na kukuuliza hivyo, inabidi uwe na sababu nzuri sana ya kukataa.”

Ameendelea kusema kubwa “Nimevutiwa kuangalia kazi za wenzangu wote. Nadhani bila mashirika ya kibinadamu kufanya kazi, mambo yatakuwa mabaya zaidi. Kwa maana hiyo, ni jambo la kuthawabisha kitaaluma.”

Lazima niseme nimekuwa na bahati kubwa na bosi wangu. Moja ya ushauri wangu bora kwa vijana wenzangu ambao wakati mwingine huja kwangu na kuniuliza ni nini ushauri wako katika suala la utendaji bora wa kazi? 

Nawajibu kuwa moja ya vidokezo bora ni kuchagua bosi mzuri sana. Nenda ukamfanyie kazi mtu unayempenda sana.

Mark Lowcock na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wakiingia katika Hospital ya mafunzo ya Kassala nchini Sudan
OCHA
Mark Lowcock na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wakiingia katika Hospital ya mafunzo ya Kassala nchini Sudan

Lowcock amesema“ Nimekuwa na bahati nzuri sana kufanya kazi kwa António Guterres. Yeye ni mtu mwenye busara sana, na ni mtu mzuri sana, mzuri sana wa kufanya kazi kama meneja. Yuko wazi kwa kile anachotaka. Ana orodha iliyo wazi ya maadili. Anatarajia uyazingatie na anakuwezesha kuendelea nayo.”

QUOTE: Moja ya vidokezo vyangu bora kwa wenzangu wachanga ni kwenda kufanya kazi kwa mtu unayempenda sana.

Nina siku nyingi, nyingi nimekuwa nikifanya kazi hii ilibidi niende kwake na kuomba msaada kidogo juu ya mada, na kila wakati nimekuwa nikishangazwa na jinsi amejibu haraka, mara moja, na jinsi jibu lake lilivyo daima imekuwa.

Je! Kuna ushauri wowote ambao ungempa mrithi wako?

Mark Lowcock: Kweli, mrithi wangu kwa bahati nzuri ni mtu mzoefu sana, ambaye nadhani labda anajua mengi zaidi juu ya mfumo wa misaada ya kibinadamu wa kimataifa kuliko mimi, kwa hivyo sidhani anahitaji ushauri kutoka kwangu.

Ni wazi, mimi na Martin tunajuana vizuri. Tumefanya kazi pamoja kwa karibu sana kwa ajili ya Yemen kwa miaka mitatu sasa. Mimi na yeye tumekuwa na majadiliano mengi.

Mark Lowcock, (kulia) Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya dharura na misaada ya kibinadamu wakati wa ziara  yake Sudan Kusini, na pichani akizungumza na mmoja wa wahudumu wa afya katika hospitali ya mafunzo ya Kassala
OCHA/Saviano Abreu
Mark Lowcock, (kulia) Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya dharura na misaada ya kibinadamu wakati wa ziara yake Sudan Kusini, na pichani akizungumza na mmoja wa wahudumu wa afya katika hospitali ya mafunzo ya Kassala

Ameniuliza maswali mengi juu ya kile kinachoendelea ili aweze kujiandaa kuchukua kazi hiyo. Nitakuwa nikitazama kutoka pembeni. Nitakuwa nikishangilia mashirika yote ya kibinadamu. 

Ikiwa kuna njia ambazo ninaweza kutoa maoni au ushauri au kuchangia, ninafurahi kufanya hivyo. Lakini najua kuwa OCHA na mfumo wa usaidizi wa kibinadamu utakuwa katika mikono mizuri sana chini ya uongozi wa Martin kama mratibu mpya.