Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO na IPC kushirikiana kuwasaidia wanamichezo walemavu

Ibrahim Al Hussein kutoka kundi la wanamichezo wakimbizi  wenye ulemavu, mzaliwa wa Syria. Alipoteza mguu wake kwenye vita nchini Syria kwasasa anaishi nchini Greece na anashiriki mashindano ya kuogelea
Milos Bicanski

Afya

Shirika la Afya ulimwenguni WHO na shirika la kimataifa la walemavu IPC hii leo wametiliana saini makubaliano ya kufanya kazi pamoja katika kukuza usawa na kuheshimu tofauti zilizopo baina ya watu katika mipango inayohusu afya na michezo kwa kila mtu, kila mahali. 

Mashirika hayo mawili yamesaini makubaliano hayo mjini Tokyo, Japan ambapo watashirikiana katika kuboresha na kuhakikisha kuna upatikanaji wa vituo bora wa ushauri wakisaikojia na huduma za kusaidia watu wenye ulemavu kupata usaidizi kwa kutumia teknolojia za kisasa za usaidizi unaoweza kubadili maisha yao ulimweguni kote na kuweka sharti la kutoa fursa sawa na ushiriki katika michezo kwa watu wenye ulemavu, ikijumlisha wanariadha wanaoshiriki michuano ya olimpiki ya watu wenye ulemavu.

“Michezo na afya ni washirika wa asili, na wanafaida zinazosaidia pande zote” amesema Dkt. Tedros Ghebreyesus Mkurugenzi Mkuu wa WHO na kuongeza kuwa “Michezo ya walemavu ni ujumbe unaotia moyo kwamba watu wenye ulemavu wanaweza kufanikiwa. Tunatumaini ushirikiano huu kati ya WHO na IPC utakuwa jukwaa kwa watu wengi wenye ulemavu kushiriki kwenye michezo, lakini pia kuonesha ulimwengu kwanini huduma za afya ni muhimu sana, kuhakikisha kila mtu anapata uangalizi wa huduma bora na kwa teknolojia wanayohitaji ili kutimiza uwezo wao.”

Naye rais wa IPC, Andrew parsons amesema “ushirikiano huu utanufaisha sana jamii, sababu michezo ni nyenzo kubwa yakuhakikisha katika jamii watu wanaishi maisha mazuri na yenye afya. Ushirikiano wa IPC na WHO unaenda zaidi ya kukuza mitindo ya kuishi na afya, na pia itazingatia jukumu la teknlojia inavyoweza kusaidia kutengeneza ulimwengu jumuishi, hususan ukizingatia uwepo wa zaidi ya watu bilioni moja wenye ulemavu ulimwenguni.”

Michuano ya olimpiki kwa watu wenye ulemavu inatarajiwa kuanza tarehe 25 Agosti na kumalizika tarehe 5 Septemba mwaka huu 2021mjini Tokyo, Japan. 

Ibrahim Al Hussein kutoka kundi la wanamichezo wakimbizi  wenye ulemavu, mzaliwa wa Syria. Alipoteza mguu wake kwenye vita nchini Syria kwasasa anaishi nchini Greece na anashiriki mashindano ya kuogelea
Milos Bicanski
Ibrahim Al Hussein kutoka kundi la wanamichezo wakimbizi wenye ulemavu, mzaliwa wa Syria. Alipoteza mguu wake kwenye vita nchini Syria kwasasa anaishi nchini Greece na anashiriki mashindano ya kuogelea

  Takwimu za watu wenye ulemavu duniani 

Ulemavu ni suala la afya kwa umma ulimwenguni kote, nchi zenye kipato cha chini kumekuwa na changamoto kwenye upatikanaji wa huduma za afya na kiteknolojia kwa kwa ajili ya kuwasaidia walemavu.

Shirika la afya ulimwenguni linakadiria asilimia 15 ya watu wote ulimwenguni wanaishi na ulemavu, na idadi hii inaendelea kuongezeka kwasababu ya mabadiliko ya idadi ya watu pamoja na watu kuendelea kuzeeka na pia kuongezeka kwa magonjwa sugu.

Mtu 1 kati ya 2 mweney ulemavu ndio anaweza kumudu huduma za afya, pamoja na huduma zinazoendana na mahitaji ya wenye ulemavu. Na mtu 1 kati ya 10 ndio mwenye uwezo wa kupata huduma zinazoweza kumsaidia kumpa mabadiliko yanayotokana na teknolojia ya kisasa.

Janga la COVID-19 limewaweke watu wenye ulemavu katika hatari yakupata maambukizi na kupata huduma mbovu, kwasababu huduma za afya na uangalizi hazitolewa katika namna ya kuwawezesha walemavu kuzipata kwa njia za urahisi.