Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Simulizi ya bibi chanjo: mkunga anayesimamia chanjo kwa watoto

Mtoto akiwekewa alama kwenye kucha yake, alama ya kuonesha amepewa chanjo huko Maiduguri, Borno, Nigeria.
UNICEF/Page
Mtoto akiwekewa alama kwenye kucha yake, alama ya kuonesha amepewa chanjo huko Maiduguri, Borno, Nigeria.

Simulizi ya bibi chanjo: mkunga anayesimamia chanjo kwa watoto

Afya

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Nigeria kwakutambua umuhimu wakutoa chanjo kwa watoto wachanga ili kuweza kuwapatia kinga ya maradhi mbalimbali wametoa ufadhili wa majokofu yanayotumia umeme wa jua katika jimbo la Imo ili kuwawezesha wauguzi kutoa huduma ya chanjo kwa watoto wachanga ammbao wengi wao walikuwa wakikosa huduma hiyo kwa muda stahidi kutokana na changamoto za miundombinu.

Asubuhi kumekucha na jogoo amewika, Margaret Uwakwe au waweza kumuita bibi chanjo , kwa taaluma ni muuguzi  lakini pia ni Afisa anayesimamia wauguzi na ugawaji wa chanjo kwenye jamii zilizopo kwenye wilaya ya Ahiazu Mbaise jimboni Imo nchini Nigeria.

Video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto- UNICEF inamuonesha akianza Siku yake kwa sala na kisha hufanya shughuli za nyumbani alafu huyooooo anajiandaa  na kupanda pikipiki tayari kwenda kwenye kituo chake cha kazi, kazi yake kubwa ni kuhakikisha watoto wachanga wa wilaya yake wanapata chanjo.

Kwakuwa yeye ndio mkuu wa kitengo chake, afikapo kazini hujadiliana na wafanyakazi wenzake na kisha kuamua kituo cha afya watakachoenda kukitembelea ambacho siku hiyo kina shughuli ya kutoa chanjo kwa watoto. Lakini kabla ya kwenda huko huakikisha kuna idadi inayohitajika ya chanjo kwa vituo vilivyoomba ndani ya wilaya yake.

Afikapo katika vituo alivyochagua kutembea kwa siku husika, hupitia makablasha na kujiridhisha shughuli zote zinafanyika kwa mujibu wa taratibu za ukunga na kuhakikisha wamama waliowaleta watoto wao hawana wasiwasi wowote kwa watoto wao kupatiwa chanjo pamoja na kuzingatia sheria za kujikinga na janga la Corona.

Pamoja na kuipenda kazi yake na kuhudumia watoto wachanga nchini Nigeria kwa moyo mkunjufu lakini Margaret anasema hii kazi inachangamoto zake.

“Changamoto yetu kubwa ni namna ya kuzunguka, hatuna magari ,tuliwahi kuwa na gari,  lakini kipindi cha mlipuko wa homa ya mafua waliondoka na gari letu la kubebea wagonjwa. Na tangia hapo tumekuwa tukitumia usafiri wa umma. Saa nyingine tunakodi gari lakini muda mwingine tunatembea kwa miguu."

Changamoto nyingine ni uwezo wa kuendesha kitengo chao,  hawana fedha za kuendesha kitengo cha kutoa chanjo kwahiyo, hata vituo vya afya pia vinapata ugumu wakuja wilayani kuchukua chanjo zao kwa sababu ya kukosa usafiri. UNICEF inaona hili na kulipatia suluhu.

“Namshukuru Mungu, Nashukuru UNICEF pamoja na vitengo vingine vya afya vya serikali, hivi karibuni walitupatia majokofu yanayotumia umeme wa jua kwenye vituo vyetu vingi vya afya kwahiyo sasa vituo vya afya vinakusanya chanjo zao na kuzihifadhi kwenye majokofu yao yanayotumia umeme wa jua na hii inafanya zoezi lao la kutoa chanjo kwa wateja wao kuwa rahisi kwa siku au kila wiki kutokana na uhitaji."

Sasa watoto wachanga katika jimbo la IMO, wana uhakika wakupata chanjo. Na Margaret anafurahia kutoa huduma kwa wakati na ubora.