Watu milioni 25 kuchanjwa dhidi ya homa ya manjano Nigeria:WHO

Shirika la Aflya ulimwenguni WHO kwa ushirikiano na serikali ya Nigeria, wamezindua kampeni kabambe na kubwa kuwahi kufanyika ya chanjo dhidi ya homa ya manjano kwa mwaka wa 2018 ikiwa na lengo la kuwafikia watu wapato milioni 25 kazikazini mwa Nigeria.

Kampeni hiyo iliozinduliwa rasmi hii leo ni moja ya kampeni za kimataifa kusuhu chanjo ya homa ya manjano kwa udhamini na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani UNICEF pamoja na GAVI unaolenga haswa majimbo ya kazikazini mwa Nigeria ya kogi, kwara na Zamfara, na baadae Borno.
Dr.Faisal Shwaib ambaye ni mkurugezi wa shirika la huduma ya afya nchini humo amesema kampeni hiyo ina lengo la kupunguza makali na pia mambukizi ya homa ya manjano nchini Nigeria kwa asilimia 90 ikipakpo mwaka 2026.
Aidha amesema homa ya manajano ambayo huambukizwa kwa njia ya mbu , imeshamiri sana katika nchi za Afrika zilizoko kusini mwa jangwa la Sahara ambapo mwaka 2017, nchini Nigeria kumekuepo na visa 358 vya homa hiyo na kuwatu 45walipoteza maisha katika majimbo 16.
WHO imekua msatari wa mbele katika kutoka mafunzo kwa wafanya kazi wa mashirika ya afya ili kuweza kukabiliana na visa vinavyojitokeza kila siku kuhusu vya homa ya manjano nchini Nigeria na barani Afrika.