Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Suluhisho pekee la migogoro na vita ni kuizuia:Amina J Mohammed

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed akihutubia katika katika chuo kikuu Mjini Abuja nchini Nigeria
UNIC Lagos/Oluseyi Soremekun
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed akihutubia katika katika chuo kikuu Mjini Abuja nchini Nigeria

Suluhisho pekee la migogoro na vita ni kuizuia:Amina J Mohammed

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J Mohammed amesisitiza umuhimu wa mtazamo wa kuzuia, katika kutatua changamoto za migogoro na vita kote duniani akisema “Suluhisho pekee na endelevu kwa changamoto za migogoro ni kuzuia. Kuzuia kutatusaidia kunyoosha pindo lililopo sasa la vita na machafuko na hivyo kutoa fursa kwa nyenzo zetu za kudhibiti maigogoro ambazo mara nyingi zinazidiwa uwezo.” 

Bi. Amina ameyasema hayo wakati akizungumza katika chou kikuu cha Baze nmjini Abuja Nigeria katika mada isemayo “Matumizi ya makubaliano ya amani katika kuepuka kuongezeka kwa vita vya siilaha.” 
Kulingana naye, kiini cha njia hii ni hitaji la kushiriki mapema na kwa bidii na wahusika mbalimbali, haswa nchi, mashirika madogo na asasi za kiraia, wakati tunaendelea kufanya uwekezaji mkubwa wa kisiasa katika ujenzi wa amani na utatuzi wa mizozo dunia. 

“Hakuna mahali popote ambapo hii ni dhahiri zaidi kuliko Afrika, ambapo Umoja wa Mataifa umeanzisha ushirikiano wa kimkakati na Muungano wa Afrika (AU) na tume ya uchumi ya Kikanda ya Umoja wa Mataifa (UNECA). Umoja wa Mataifa pia umejikita katika kusaidia kuimarisha uwezo wa kitaifa wa kuzuia mizozo, kwa ufahamu kwamba kinga ni bora wakati inaongozwa na watendaji wa kitaifa au wa ndani ", amesema Bi. Mohammed Umoja wa Mataifa, Bi Mohammed amesema umeweka ujumuishaji na kukuza ushiriki wa kisiasa wa wanawake na ushiriki wa vijana, katikati ya juhudi zake zote kuelekea amani na usalama wa kudumu. 
Tutoe kipaumbele kwa usawa wa kijinsia 
 

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed akipiga picha na wasichana Katika Chuo kikuu za Baze huko Abuja nchini Nigeria
UNIC Lagos/Oluseyi Soremekun
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed akipiga picha na wasichana Katika Chuo kikuu za Baze huko Abuja nchini Nigeria

Katika kuanzisha jukumu la usawa wa kijinsia katika utatuzi wa mizozo na ujenzi wa amani, Bi Mohammed amesisitiza kuwa usawa wa kijinsia lazima upewe kipaumbele, akibainisha kuwa jamii ambazo zinaacha nusu ya watu wao nyuma katika maisha ya kisiasa na uchumi, uongozi na uamuzi, zitakuwa hatarini kwa mizozo.  
"Jitihada ambazo zitashughulikia mahitaji na haki maalum za wanawake na wasichana zinaweza kuwa na athari nzuri zaidi na kuchangia vyema katikam amani endelevu." Ameongeza Naibu Katibu Mkuu. 

Alipowasili katika chuo kikuu hicho, alipokelewa na makamu mkuu, wa chuo Profesa Tahir Mamman (OON, SAN); Waziri wa uchukuzi wa Nigeria, mstaafu  Mhe. Chibuike Rotimi Amaechi, Mkuu wa Kitivo cha sheria, Dkt. Ali Ahmad na mameneja wengine wakuu wa chuo kikuu hicho