Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Makao makuu ya mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai, ICC huko The Hague, Uholanzi

Mwendesha Mashtaka Mkuu Mpya wa ICC aapishwa Rasmi

UN /Rick Bajornas
Makao makuu ya mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai, ICC huko The Hague, Uholanzi

Mwendesha Mashtaka Mkuu Mpya wa ICC aapishwa Rasmi

Amani na Usalama

“Naapa kwamba nitatekeleza majukumu yangu kwa Mamlaka yangu ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Kamosa ya Jinai kwa heshima, uaminifu, bila upendeleo na kwa dhamiri, nitaheshimu usiri kwenye kufanya uchunguzi na kuendesha mashtaka” kiapo cha Mkuu mpya wa ICC

 

Maneno ya Karim Asad Ahmad Khan QC aliyosema hii leo wakati akiapa rasmi kuwa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai – ICC, katika Makao Makuu ya Mahakama hiyo yaliyopo The Hague, nchini Uholanzi. 
Khan, raia wa Uingereza na Kaskazini mwa Ireland alichaguliwa huko mjini New York mwezi February mwaka huu 2021, kushika wadhifa huo wa ICC kwa miaka 9 akichukua nafasi ya Bi. Fatou Bensouda aliyemaliza muda wake rasmi hapo jana.
Sherehe za uapisho huo ziliongozwa na Rais wa ICC, Jaji Piotr Hofmanski ambaye katika hotuba yake alimpongeza na kumkaribisha rasmi ICC huku alitilia mkazo jukumu muhimu la mwendesha mashtaka. 
“Ingawa Majaji ndio wenye jukumu la kufanya maamuzi katika kila kesi, lakini ni ukweli kuwa hizo kesi zisingewafikia majaji bila ya uamuzi wa Mwendesha Mashtaka kuwaleta watuhumiwa mahakamani. Na Mwendesha Mashtaka ndio mwenye jukumu la kufanya uchunguzi wa awali, kufanya uchunguzi na mashtaka, na maamuzi ya uchaguwaji wa Ushahidi wa mashtaka na kuwasilishwa.” 
Naye makamu wa Rais wa Baraza la Nchi Wanachama, Balozi Katerina Sequensova akizungumza kwa niaba wa Rais wa Baraza hilo, amesema anaamini Bwan Khan anaingia kuchukua wadhifa huo akiwa na uzoefu wa kutosha kwenye masuala ya jinai ya kimataifa na kwamba anauhakika atazingatia misingi ya  kuleta haki.