Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bado tunawasaka wanakijiji  waliokimbilia msituni baada ya kuvamiwa Bahr Ole Payam:UNMISS

Watu waliofurushwa makwao wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo mabadailiko ya tabianchi.
IRIN/Jacob Zocherman
Watu waliofurushwa makwao wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo mabadailiko ya tabianchi.

Bado tunawasaka wanakijiji  waliokimbilia msituni baada ya kuvamiwa Bahr Ole Payam:UNMISS

Amani na Usalama

Machafuko na utekaji nyara unaofanywa na vikundi vya watu wenye silaha umewafanya baadhi ya wananchi kuyakimbia makazi yao na kuishi msituni ili kunusuru maisha yao nchini Sudan Kusini. Kwa mujibu wa mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo UNMISS kimewasaka bila mafanikio wanakijiji wa Bahr Ole Payam waliokimbilia msituni baada ya kuvamiwa hivi karibuni na maeneo yao kuchomwa moto huku watu watatu wakipoteza maisha.

Hali ni bayana majivu kila kona, si kwenye magari yanayotumiwa na walinda amani, si nyumba wanazoishi wananchi wa kijiji hiki wala sufuria zao wanazotumia kupikia chakula, kilichobaki ni masalia yaliyoshemeni jivu baada ya majibizano makali yaliyofanywa na vikundi vyenye silaha vilivyo vamia katika eneo hili 

Uvamizi huo umesababisha vifo vya watu watatu wawili kati yao wakiwa ni wanajeshi wa mmoja ni rai na kuleta hofu miongoni mwa wakazi wa eneo hili ambao wameamua kukimbilia msituni katikati ya kaunti ya Juba- Maridi barabara ya Equotoria Magharibi kuokoa ili kuokoa maisha yao ambapo hata askari wa kulinda amani walipokuwa wakizunguka kuwatafuta waliambulia patupu. 

Afisa wa UNMISS Yambio anayehusika na usaidizi na usalama Anthony Moudie akizungumza mara baada ya kuwasili katika eneo lililoshambuliwa anasema hali si nzuri na inahuzunisha,“Hatujui ni namna gani hawa watu wataweza kuishi. kama UNMISS tunatetea kwa niaba ya wananchi hawa wapatiwe ulinzi wa uhakika, kwasababu jukumu letu la kwanza ni kuhakikisha usalama wa raia. Tumesikia baadhi ya watu hawana makazi ya kuishi wengine wamekimbilia Mambe wakati wengine wapo tuu msituni. Baadhi wamesharudi lakini bado tutaendelea kuangalia ni namna gani ya kuwasaidia.”  

Kwa mujibu wa Chifu Bismak Baloko, Kiongozi wa wananchi wa Bahr Olo Payam, watu wengi wanahofia maisha yao ndio maana wamekimbilia msituni na kuiomba serikali ya Sudan kusini kuingilia kati na kurejesha amani katika eneo hilo.  “Kama watu wanavyosema, tunataka amani. Ni amani tuu ndio itaturejeshea furaha yetu na tutaweza kuishi vile tunavyotaka hii ndio maana kamili ya furaha kwetu. Lakini kwa hiki kinachoendelea sasa hatuko salama. Tunataka serikali ifikirie jinsi ya kupatia ufumbuzi suala hili” 

Vikundi vyenye silaha vimeendelea kufanya mashambulizi katika maeneo ya Maridi na Mundri. Tukio la hivi karibuni ni kuvamiwa kwa  kambi ya kijeshi iliyopo Bahr Olo Payam katika Kaunti ya Maridi.