Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutoka Mashinani: Manusura wa mzozo Uganda asaidia jamii kusonga mbele 

Okello anasema yeye ni miongoni mwa waliokuwa na bahati hawakutekwa na waasi wa LRA nchini Uganda.
ICC-CPI/Pete Muller
Okello anasema yeye ni miongoni mwa waliokuwa na bahati hawakutekwa na waasi wa LRA nchini Uganda.

Kutoka Mashinani: Manusura wa mzozo Uganda asaidia jamii kusonga mbele 

Haki za binadamu

Mwanaume mmoja nchini Uganda ambaye amejiepusha kutumbukia katika mzozo wa miongo kadhaa nchini humo, kwa kuepuka kutumikishwa vitani akiwa mtoto, amejitolea utu uzima wake kuleta uponyaji kwa jamii ambazo zimeathiriwa na mapigano kati ya serikali na kikundi cha waasi cha Lord’s Resistance Army, LRA. 

Watoto wapatao elfu 25, walitekwa na askari wa na kutumikishwa kama vijakazi, wakati wa mapigano kati ya serikali na LRA kuanzia miaka ya 1980. 

Okello Tito anasema yeye alikuwa “miongoni mwa waliobahatika” kwa sababu hakutekwa au kuuawa, hata kama familia yake ililazimika kukimbia nyumbani kwao usiku wa manane baada ya waasi kuitia moto nyumba yao. 

Leo, anafanya kazi kama kiongozi wa jamii huko kaskazini mwa Uganda, kitovu cha mzozo. Huko anatumia muda wake “kutuliza watu, kufanya mashauriano, kusaka suluhu na kusonga mbele”. 

Ametoa simulizi yake hii kama sehemu ya mpango unaoitwa, “Maisha baada ya mzozo”  ikijikita katika haki ya kimataifa, mpango uliozinduliwa na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai  (ICC). 

Mwaka 2004 Kaskazini mwa Uganda wasafiri wa usiku walikuwa wanaondoka majumbani mwao na kukaa makazi ya muda kwa hofu kwamba watoto hao wataingizwa kwenye LRA.
© UNICEF/Chulho Hyun
Mwaka 2004 Kaskazini mwa Uganda wasafiri wa usiku walikuwa wanaondoka majumbani mwao na kukaa makazi ya muda kwa hofu kwamba watoto hao wataingizwa kwenye LRA.

ICC yenye makao yake makuu huyo The Hague, Uholanzi, ni mahakama ya kwanza duniani kutoa hukumu dhidi ya makosa ya kikatili zaidi, ikiwemo mauaji ya kimbari, uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu. 

Siku ya Alhamisi Mei 6, 2021, mahakama hiyo itatoa hukumu dhidi ya Dominic Ongwen, kiongozi wa zamani wa LRA ambaye alipatikana na hatia ya makosa 61, kati ya mwaka 2002 – 2005, makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita wakati wa mzozo huko kaskazini mwa Uganda. 

Soma zaidi hapa kuhusu jinsi Okello Tito anajaribu kuponya jamii yake baada ya miongo ya mapigano .