Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miaka 10 ya vita Syria nusu ya raia wote wamekimbia makwao 

Mama na mwana wakitembea katika makazi yao kwenye shule iliyoharibiwa. Hawakupata hema katika kambi ya wakimbizi a ndani.
© UNOCHA/Mohannad Zayat
Mama na mwana wakitembea katika makazi yao kwenye shule iliyoharibiwa. Hawakupata hema katika kambi ya wakimbizi a ndani.

Miaka 10 ya vita Syria nusu ya raia wote wamekimbia makwao 

Wahamiaji na Wakimbizi

Ilikuwa siku, wiki, miezi na sasa imeshatimia miaka 10 tangu kuzuka vita nchini Syria na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema nusu ya raia wa nchi hiyo wamelazimika kufungasha virango na kukimbia huku jinamizi la vita hivyo likiendelea kuwaandama.

Mzozo wa Syria uliosambaratisha kila kitu kuanzia makazi , hadi maisha ya watu na kuwalazimisha mamilioni kufungasha virago kuzikimbia nyumba zao na kwenda kusaka usalama ndani na nje ya nchi bado unaendele kuleta madhila kwa raia wa nchio miaka 10 baadaye limesema shirika la UNHCR

Na kwa mujibu wa Kamishina mkuu wa shirika hilo Filipo Grandi, dunia imeiangusha serikali na watu wa Syria  kwani kwake yeye anaikumbuka miaka hii 10 ya vita kwa majonzi na huzuni kubwa huku akisema “ Kwa viongozi wa dunia maadhimisho haya ni kumbusho kwamba umekuwa ni muongo wa vifo, uharibifu na mamilioni ya watu kutawanywa mambo yaliyofanyika huku wakiyatazama.” 

Bwana Grandi amesema katika miaka 10 hii ya madhila nusu ya watu wote wa Syria wamelazimika kukimbia makwao, milioni 5.5 kati yao kuwa wakimbizi kwenye nchi za ukanda wao huku maelfu wengine wakivuka mpaka na kutawanyika katika nchi 130 duniani. 

Zaidi ya hapo raia wengine milioni 6.7 wa Syria wamekuwa wakimbizi wa ndani nchini mwao na hakuna mji wala kijiji nchini humo kilichonusurika na vita hivyo na athari za kibinadamu kwa watu waliosalia Syria hazielezeki imesema UNHCR. 

Shirika hilo la wakimbizi limeongeza kuwa na sasa janga la corona au COVID-19 limekuwa ni kama msumari wa moto juu ya kidonda. 

Katika nchi jirani ya Lebanon Wasyria 9 kati 10 wanaishi katika ufukara mkubwa, huku kushindwa kujimudu kimaisha, ongezeko la ukosefu wa ajira na janga la COVID-19 vimezitumbukiza jamii zinazohifadhi wakimbizi hao nchini Jordan, Lebanon, Uturuki na Iraq hadi chini ya msitari wa umasiki. 

Hata hivyo kwa miaka hiyo 10 UNHCR inasema imeshuhudia ukarimu wa hali ya juu kutoka kwa baadhi ya watu, nchi na mashirika wanaofanyiwa wakimbizi wa Syria na limetaka mgogoro huo unaoendelea usivunje mshikamano kwa mamilioni ya raia wa Syria wanaohitaji msaada. 

Na kwa jumuiya ya kimataifa shirika hilo limesema “Ni lazima iongeze mara mbili juhudi zake za pamoja kuweza kuwasaidia wakimbizi wa Syria na jamii zinazowa