Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema hakuna ushahidi kwamba adhabu ya kifo itakuwa na matokeo mazuri ya kupunguza vitendo vya mauaji.
Watalaam huru wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa leo wamelaani vikali hukumu ya kifo aliyopewa mhadhiri wa chuo kikuu cha Bahauddin Zakariya nchini Pakistan kwa madai ya kukashifu dini.
Ofisi ya Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu imesema imeshtushwa na kutiwa hofu kubwa na hukumu ya kifo waliyokatiwa watu 30 na mahakama ya mwanzo maalum kwa makossa ya jinai mjini Sana’a nchini Yemen.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limeelezea wasiwasi wake mkubwa juu ya ripoti za mara kwa mara za kuuawa kwa watoto kwenye mataifa ya kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, MENA.
Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet hii leo mjini Geneva Uswisi ameisihi serikali ya Brunei kusitisha utekelezaji wa sheria mpya ambayo ikiwa itatekelezwa kama ilivyo sasa, inaweza kutoa adhabu za kikatili ambazo zinakiuka sana sheria za kimataifa za haki za binadamu ikiwamo adhabu ya kifo kwa kupigwa mawe.
Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR ina wasiwasi kuhusu taarifa kutoka Misri isemayo watu 15 wamenyongwa mwezi huu wa Februari ambapo watu tisa maisha yao yalikatiliwa isiku ya Jumatano wiki hii huku wengine sita walikabiliwa na hukumu ya kifo mapema mwezi huu.
Wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameitaka serikali ya Saudi Arabia kusitisha mara moja utekelezaji wa hukumu ya kifo kwa watu sita waliohukumiwa kufa kwa madai ya kufanya uhalifu walipokuwa na umri wa chini ya miaka 18.
Kamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet hii leo mjini Geneva, Uswisi amelaani mauaji ya Zeinab Sekaanvand Lokran nchini Iran.