Shirika la Amani Girls Home limetuepusha na ukatili wa kijinsia-Wanawake Mwanza, Tanzania 

21 Disemba 2020

Shirika la Amani girls home la Mwanza Tanzania limeanzisha mradi unaowawezesha wasichana hususani wale waliokumbwa na changamoto mbalimbali za kimaisha, ili waweze kufikia malengo yao kwa kuwapa ujuzi mbalimbali.  

Kupitia shirika hili lisilo la kiserikali, baadhi ya wanawake waliokuwa na changamoto za kimaisha, wamepewa ujuzi mbalimbali na sasa wanautumia kujikwamua hasa kiuchumi na hivyo kuepuka ukatili wa kijinsi ambao moja ya visababishi vyake ni utegemezi wa kiuchumi. 

Lucy Daudi ambaye ni mnufaika wa moja ya program za shirika la Amani Girls Home, akizungumza kwa niaba ya wengine, amesema shirika hilo limemkwamua yeye binafsi na wanawake wenzake.  

Saysarah Masalu Msimamizi Msaidizi Kitengo cha Familia na Maendeleo ya Jamii wa Amani Girls Home ameeleza kwa kina shughuli zao na mafanikio.  

 

 

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter