Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kinachohitajika ni utashi wa kisiasa tu kumaliza tatizo la kutokuwa na utaifa:UNHCR 

Ukosefu wa uaifa ni changamoto inayowakumba watu wengi.
© UNDP/Mirfozil Khasanov
Ukosefu wa uaifa ni changamoto inayowakumba watu wengi.

Kinachohitajika ni utashi wa kisiasa tu kumaliza tatizo la kutokuwa na utaifa:UNHCR 

Haki za binadamu

Kamishina mkuu wa wakimbizi Filippo Grani leo ametoa wito kwa viongozi wa dunia kuchukua hatua Madhubuti ili kutokomeza tatizo la kutokuwa na utaifa ifikapo mwaka 2024. 

Katika kuadhimisha miaka 6 ya kampeni ya #IBelong yenye lengo la kutokomeza tatizo hilo la kutokuwa na utaifa ifikapo mwaka 2024 kamishina huyo ambaye pia ni mkuu wa shirika la wakimbizi duniani UNHCR ametaka juhudi ziongezwe mara mbili “kutatua changamoto hii ya kibinadamu katika ya karne ya 21.” 

Ameonya kwamba haja ya kufanya hivyo ni kubwa zaidi sasa wakati dunia imeghubikwa na janga la corona au coronavirus">COVID-19 ambalo linazidisha changamoto kwa mamilioni ya watu wasio na utaifa kote duniani. 

“Janga la COVID-19 limeonyesha kwamba sasa kuliko wakati mwingine wowote  kuna haja ya ujumuishaji na uharaka wa kutatua changamoto ya kutokuwa na utaifa. Janga hili halibagui kati ya rai ana asiye rai ana haina faida yoyote kwa mataifa, nchi au jamii kwa watu kuachwa bila utaifa na kuishi maisha ya kutengwa katika jamii” ameongeza Bwana. Grandi. 

Ingawa ni vigumu kuapata takwimu halisi kwa kuwa watu wasio na utaifa mara nyingi hawahesabiwi au kujumuishwa katika sensa , kunaweza kuwa na watu takriban milioni 4.2 wasio na utaifa katika nchi 76 kwa mujibu wa shirika la UNHCR lakini idadi kamili inatarajiwa kuwa kubwa zaidi. 

Kambi ya Kutupalong-Balukhali eneo la Cox's Bazar nchin Bangladesh ni makazi ya zaidi ya wakimbizi 600,000 wa kirohingya ambao hawana utaifa.
© UNICEF/Bashir Sujan
Kambi ya Kutupalong-Balukhali eneo la Cox's Bazar nchin Bangladesh ni makazi ya zaidi ya wakimbizi 600,000 wa kirohingya ambao hawana utaifa.

Ni rahisi kulizuia na kulitatua 

Kwa mujibu wa kamishina mkuu wa wakimbizi “Tatizo la kutokuwa na utaifa ni rahisi kuliotatua na kulizuia , kwani ni suala la utashi wa kisiasa kubadili hadhi na Maisha ya mtu, lakini bado athari za kutochukua hatua hususani katikati ya janga hili la COVID-19 zinaweza kuwa ni za kutishia uhai. Ili kulinda na kuokoa maisha haya tunatoa wito kwa serikali kutatua suala la kutokuwa na utaifa na kuhakikisha kwamba hakuna mtu anayeachwa nyuma.” 

Kampeni ya #IBelong iliyozinduliwa mwaka 2014 lengo lake lilikuwa ni kutokomeza tatizo hilo ndani ya miaka 10 kwa kuwabaini na kuwalinda watu wasio na utaifa, kushughulikia hali zilizopo na kuzuia kutokea kwa watu wapya wasio na utaifa. 

Kampeni hiyo pia inahusiana moja kwa moja na kipengele cha 9 cha lengo namba 16 la mawndeleo endelevu (SDG16) cha kutoa hadhi ya utaifa kisheria kwa wote ikiwemo vyeti vya kuzaliwa ifikapo mwaka 2030. 

COVID-19 yazidisha hatari kwa wasio na utaifa 

Kutokuwa na utaifa ni tatizo linalotatulika na kuzuilika, ni suala la utashi wa kisiasa kubadili hadhi ya mtu- Kamishina Grandi 

Wakati kumepigwa hatua kubwa katika kupunguza watu wasio na utaifa kote duniani tangu kuzinduliwa kwa kampeni mwezi Novemba mwaka 2014, hivi sasa janga la COVID-19 limeongeza changamoto na kukosa haki kunakowakabili watu wasio na utaifa. 

Kukosa haki muhimu za kisheria na mara nyingi kushindwa kupata fursa za huduma muhimu watu wengi wasio na utaifa wanajikuta wametengwa kisiasa na kiuchumi, wanabaguliwa na kuwa katika hatari ya kunyanyaswa na kufanyiwa ukatili. 

Katika nchi nyingi watu wasio na utaifa wakiwemo wakimbizi wanaishi katika Maisha duni na mazingira mabaya ya usafi ambayo yanaweza kuwaongezea hatari ya magonjwa. 

“Bila uraia watu wengi wasio na utaifa hawana fursa au hawajumuishwi katika huduma za msingi za afya ya umma na hifadhi ya jamii. Wameachwa katika hatari kubwa wakatu huu wa janga la COVID-19” amesema Grandi. 

Hata hivyo ameongeza kuwa baadhi ya nchi zimeonyesha uongozi imara kwa kujumuisha watu wasio na utaifa katika mikakati yao ya kupambana na COVID-19, kuhakikisha kwamba wanapata fursa za kupimwa na kutibiwa, chakula, nguo na barakoa. 

Nchi nyingine zimefanya usajili wa kuzaliwa na aina zingine za nyaraka za kiraia kuwa ni huduma ya msingina kuendelea na operesheni licha ya COVID-19 na hivyo kusaidia kuzuia maambukizi mapya kuongezeka miongoni mwa wasio na utaifa.