Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutoka kuwa mkimbizi hadi kuajiriwa na kampuni ya kutumia ndege zisizo na rubani 

Ndege zisizo na rubani hupachikwa programu ambazo zinafuatilia masuala  yanayoathiri ustawi wa binadamu
WeRobotics
Ndege zisizo na rubani hupachikwa programu ambazo zinafuatilia masuala yanayoathiri ustawi wa binadamu

Kutoka kuwa mkimbizi hadi kuajiriwa na kampuni ya kutumia ndege zisizo na rubani 

Wahamiaji na Wakimbizi

Mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC amekuta ndoto zake zikitimia baada ya kupata mafunzo katika Chuo cha Afrika kinachofundisha masuala ya ndege hizo pamoja na uchambuzi wa data.

Huyo ni Regeza, mkimbizi kutoka DR Congo ambaye sasa anaishi katika kambi ya wakimbizi ya Dzaleka nchini Malawi. Yeye aliwasili kambini hapa mwaka 2016 akisema kuwa miezi miwili ya mwanzo ilikuwa ni changamoto kubwa kwake kwa sababu ya lugha.  

Regeza anafahamu kifaransa, ilhali Malawi lugha zinazotumika ni Chichewe na Kiingereza. 

Akiwa kambini Dzaleka, alihitimu mafunzo ya lugha kwa njia ya mtandao na kupata diploma na kisha alihitimu shahada ya kwanza kwa njia ya mtandao,“Nilipata fursa ya kujiandikisha na Chuo cha Afrika cha ndege zisizo na rubani, ADDA kupitia udhamini wa chuo cha ufundi cha Virginia kwa msaada wa UNICEF hapa Malawi. Mtaala wao ni miezi mitatu ambapo tunajifunza teknolojia ya ndege zisizo na rubani, uchambuzi wa data na tukapatiwa vyeti.” 

Sasa ndoto za Regeza zimetimia kwa kuwa amepata vyeti vitatu vinavyomwezesha kufanya kazi na kampuni ya Swoop Aero nchini Malawi na pengine Msumbiji na DR Congo na hutumia ndege zisizo na rubani kukusanya sampuli za damu na kuziwasilisha vituo vya afya vilivyoko mbali nchini Malawi. 

Hata hivyo zaidi ya yote,  “Nataka kujifanyia kitu na pia kuonesha wakimbizi wenzangu kuwa tunaweza kuwafanya kitu. Na kwamba kuna watu wanawafikiria wao na ustawi wao na kwamba wanaweza kupeleka kitu kuwasaidia.”