Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maafisa wa ngazi za juu wa UN wenye asili ya Afrika watoa wito wa mapambano zaidi kumaliza ubaguzi wa rangi

Kumbukumbu ya kifo cha George Floyd aliyeuawa na polisi
Hazel Plunkett
Kumbukumbu ya kifo cha George Floyd aliyeuawa na polisi

Maafisa wa ngazi za juu wa UN wenye asili ya Afrika watoa wito wa mapambano zaidi kumaliza ubaguzi wa rangi

Haki za binadamu

Kundi la zaidi ya viongozi 20 wakuu wa Umoja wa Mataifa ambao wanaripoti moja kwa moja kwa Katibu Mkuu Antonio Guterres, na ambao ni waafrika au wenye asili ya Afrika, wameorodhesha na kutia saini taarifa ambayo imechapishwa Ijumaa ikieleza kuchukuzwa kao na ubaguzi unaoenea, wakionesha hitaji la 'kwenda mbali zaidi na kufanya zaidi' kuliko kulaumu tu.

Waliotia saini ni pamoja na viongozi wa ngazi za juu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa kama vilev Dkt Tedros Ghebreyesus ambaye ni Mkuu wa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO, Winnie Byanyima Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS na Natalia Kanem wa UNFPA.

Andiko hilo linaanza kwa kukumbusha kifo cha George Floyd, Mmarekani Mweusi ambaye alifariki baada ya afisa polisi wa Minneapolis alimkandamiza shingoni kwa goti kwa takribani zaidi ya dakika nane. Sehemu ya andiko inasema, “kupigania pumzi, kuomba huruma. Dunia nzima ilikisikia kilio hicho cha kusikitisha.”

Aidha andiko likigusia “mateso ya vizazi” ambayo yanatokana na ukosefu wa haki hasa dhidi ya watu wenye asili ya Afrika, sehemu ya maoni yaliyoandikwa na viongozi wenyewe, inatangaza kuwa sasa ni wakati muafaka kwenda mbali zaidi ya kulaumu tu matendo dhidi ubaguzi wa rangi, ambao wanaueleza kama “janga la ulimwengu ambalo limetekelezwa kwa karne nyingi.”

Ni wakati wa kuchukua hatua

Viongozi hao wametoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuchukua hatua za kusaidia kukomesha ubaguzi wa rangi ulioratibiwa dhidi ya watu wa asili ya Afrika na makundi mengine ya watu wachache.

Wakitambua juhudi za Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kushughulikia suala la ubaguzi wa rangi wa kimfumo katika ngazi zote, ikiwemo ndani ya Umoja wa Mataifa, waandishi wa andiko hilo wameeleza kuwa Umoja wa Mataifa unapaswa kuongozwa kwa mfano kwa tathmini ya jinsi tunavyoshikilia mkataba wa Umoja wa Mataifa ndani ya taasisi yetu.”

Wajibu wa kuongea

Viongozi hao wa kiafrika wamesema msimamo wa o wa kuungana na wandamanaji wa amani kama vile maandamano yaliyoandaliwa na Black Lives Matter au makundi mengine wakipigania haki na pia maandamano mengine ya ubaguzi wa kimfumo na ukatili wa polisi, ilikuwa ni “kuonesha majukumu yetu na wajibu wetu kama wafanyakazi wa umma wa kimataifa kusimama na kusema dhidi ya ukandamizaji.”

Andiko la viongozi hao linakamilika kwa kunukuu baadhi ya maoni ya wanaharakati wa haki za binadamu akiwemo Martin Luther King, Nelson Mandela, na Askofu Desmond Tutu, nukuu inayosema “ukombozi wa mtu mweusi ni muhimu kabisa kwa ukombozi wa mtu mweupe: hakuna atakayekuwa huru hadi pale wote tutakapokuwa huru.”

Viongozi waliotia saini ni

  • Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa WHO
  • Mahamat Saleh Annadif, Mkuu wa MINUSMA
  • Zainab Hawa Bangura, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya UN mjini Nairobi Kenya
  • Winnie Byanyima, Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS
  • Mohamed Ibn Chambas, Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa na Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa Afrika ya Magharibi na Saleh (UNOWAS)
  • Adama Dieng, Mshauri Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu uzuiaji wa mauji ya kimbari
  • François Lounceny Fall, Mkuu wa Ofisi ya kanda ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Afrika ya Kati.
  • Bience Gawanas, Mshauri Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya Afrika.
  • Gilbert Houngbo, Rais wa mfuko wa kimataifa kwa ajili ya maendeleo ya kilimo IFAD
  • Bishar A. Hussein, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la posta duniani, UPU
  • Natalia Kanem, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu, UNFPA
  • Mukhisa Kituyi, Katibu Mkuu wa mkutano wa kimataifa wa maendeleo na biashara UNCTAD
  • Kingsley Mamabolo, Mkuu wa ujumbe wa pamoja wa Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa Darfur Sudan, UNAMID.
  • Phumzile Mlambo-Ngcuka, Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN Women
  • Mankeur Ndiaye, Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jamhuri ya Afrika ya kati
  • Parfait Onanga-Anyanga, Mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Pembe ya Afrika
  • Moussa D, Oumarou, Naibu Mkurugenzi Mkuu, Shirika la kazi duniani ILO
  • Pramila Patten,Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu unyanyasaji wa kingono katika maeneo ya migogoro
  • Vera Songwe, mkuu wa tume ya Umoja wa Mataifa ya uchumi kwa ajili ya Afrika ECA
  • Hanna Tetteh, Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Muungano wa Afrika
  • Ibrahim Thiaw, Mkuu wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa kudhibiti kuenea kwa jangwa, UNCCD
  • Leila Zerrougui, Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini DRC ambaye pia ni mkuu wa MONUSCO