Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kemikali za sumu kwenye mazao ni ‘mwiba’ kwa asali bora

Nyuki ni wadudu muhimu sana, bila uwepo wao maua hayatachavuliwa na upatikanaji wa chakula utakuwa hatarini.
FAO
Nyuki ni wadudu muhimu sana, bila uwepo wao maua hayatachavuliwa na upatikanaji wa chakula utakuwa hatarini.

Kemikali za sumu kwenye mazao ni ‘mwiba’ kwa asali bora

Ukuaji wa Kiuchumi

Kuelekea siku ya nyuki duniani kesho tarehe 20 mwezi Mei, wafugaji wa nyuki nchini Tanzania wamezungumzia umuhimu wa wakulima kuepuka kutumia kemikali za sumu ili kuhakikisha asali ya nyuki haina madhara yoyote kwa afya ya binadamu.

Frederick Katulanda ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa waandishi wa habari wa ufugaji nyuki wilaya ya Misungwi, mkoani Mwanza, amesema hayo akihojiwa na kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa, UNIC Dar es salaam, akieleza kuwa hiyo ni moja ya changamoto wanazopata kwenye ufugaji.

Licha ya asali, mazao mengine ya nyuki ambayo tunaweza kuyachakata ni nta na tunaichakata kwa kutengeneza  mishumaa pekee yake, lakini matumizi mengine kama kutengeneza gundi, kutengeneza dawa ya kunga'rishia viatu, kutengeneza pengine mafuta au sabuni na manukato kwa ajili ya hizi nta bado hatujafikia. Kwahivyo iwapo watu wengi watajitokeza  viwanda vingi vya kuchakata mazao ya asali basi kuna uwezekano mkubwa wa kuongeza ajira nyingi kupitia sekta hii ya asali na kuliletea taifa mapato makubwa sana

Bwana Katulanda akaenda mbali zaidi kutoa wito kwa wawekezaji hususan katika kuwezesha kunufaika zaidi na mazao ya asali akisema kuwa, 

Hizi dawa zinaathiri sana ukuaji wa nyuki lakini pia zinasababisha sisi wavunaji wa asali tupate asali ambayo haifai katika soko la  kimataifa  kwasababu  unapolima kwa mfano nyanya au pamba  unapulizia dawa nyuki wanakwenda kuchukua yale maua kwa ajili ya kupata poleni au poleni ikiwa na   viambato vya sumu sasa hii poleni nyuki wanaitumia kutengenezea asali na kama watachukua poleni ambayo maua yake yamepuliziwa dawa maana yake ni kwamba tutazalisha  asali yenye dawa na itakuwa ni asali isiyofaa kwa matumizi ya binadamu