Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhuru wa vyombo vya Habari ni chachu ya kukabili COVID-19 na taarifa potofu:UN

Nembo ya siku ya uhuru wa vyombo vya Habari duniani
UNESCO
Nembo ya siku ya uhuru wa vyombo vya Habari duniani

Uhuru wa vyombo vya Habari ni chachu ya kukabili COVID-19 na taarifa potofu:UN

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Waandishi wa Habari ni kitovu cha kukabiliana na mlipuko hatari wa taarifa potofu zinazoambatana na janga la virusi vya corona au COVID-19 amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Msataifa leo katika mazungumzo kwa njia ya mtandao ya kuchagiza uhuru wa vyombo vya Habari wakati huu wa mgogoro wa kimataifa.

  “Dawa mujarabu ya janga hili la taarifa potofu ni kutoa Habari na tathimini sahihi zinazoambatana na Ushahidi. Inategemeana na uhuru wa vyombo vya Habari na uhuru wa kutoa taarifa.”Amesema mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa.
Majadiliano hayo yameandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO kwa ajili ya kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya Habari ambayo kila mwaka huadhimishwa Mei 3.
Washii walikuwa Pamoja na waandishi wa Habari na wataalam wa Habari kutoka kote duniani Pamoja na wawakilishi wa serikali na makampuni ya Habari za mitandao ya kijamii

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres  akizungumza na vyombo vya habari baada ya kutembelea msikiti wa Al Noor katika mji wa Christchurch, New Zealand.
UN Photo/Mark Garten)
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akizungumza na vyombo vya habari baada ya kutembelea msikiti wa Al Noor katika mji wa Christchurch, New Zealand.

Ukweli, majeruhi wa kwanza wa janga hilo
Akinukuu usemi maarufu wa kitambo mkuu wa UNESCO Audry Azoulay ameeleza kwamba “kama ilivyokuwa wakati wa vita, ukweli unawezakuchukuliwa kama majeruhi wa kwanza wa janga la corona”.
Ametoa wito kwa watu wote kila mahali kutetea na kuheshimu uhuru wa vyombo vya Habari na kutoingiliwa. Amesema pia ni muhimu kwamba vyombo vya Habari vikatambua kwamba vina wajibu wa kuhakikisha ukweli wa taarifa zinazotoa kitu ambacho kinapaswa pia kwa vyombo vya mitandao ya kijamii na kidijitali.
Amesisitiza kwamba “Katika wakati wa uvumi na taarifa potofu, ni lazima wote tujifunze kutumia nguvu kuchagiza ukweli, kuthibitisha takwimu na uhuru wa vyombo vya Habari kote duniani. Nina furaha pia kuona Zaidi na Zaidi mitandao ya kijamii inachukua hatua dhidi ya taarifa potofu kama wanavyopaswa na kunastahili kuwepo na utaratibu na sio wakati tu wa mgogoro wa kimataifa” amesema Bi. Azoulay.


UN inapambana na taarifa potofu kuhusu COVID-19
Katika hotuba yake Mkuu wa Umoja wa Mstaifa ameelezea jinsi gani shirika hilo la kimataifa linachukua hatua kukabiliana na kile ambacho shirika lake la afya duniani WHO ilichokiita “taarifa za kuelimisha kuhusu gonjwa huo”. Kwa mfano Umoja wa Mataifa unafanyakazi na mitandao ya kijamii kuchagiza jinsi gani watu wanaweza kujilinda , kuwa salama na kusalia na afya njema, lakini pia linakabiliana na taarifa za uongo na potofu kwa kuweka bayana taarifa za uhakika na sayansi. “Mashirika ya kimataifa Pamoja na serikali vinajukumu kubwa katika kuchagiza ukweli na mitazamo ya kisayansi”, ameongeza mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa . Hata hivyo amesisitiza kwamba hakuna yeyote wakati huu wa janga la corona ambaye anaweza kuchukua nafasi ya vyombo vya Habari katika kutoa taarifa na uchambuzi kwa umma na kukanusha uvumi na upotoshaji.
 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akizungumza na vyombo vya habari mjini Benghazi.
UN Libya
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akizungumza na vyombo vya habari mjini Benghazi.

 

 


Waandishi wa Habari wako katika tisho kubwa
Katibu Mkuu amewashukuru waandishi wa Habari na wengine wanaofanyakazi katika vyombo vya Habari kama wale ambao wanahakiki ukweli wa taarifa na kuchapisha kwenye mitandao ya kijamii. Pia amesema ukiacha mbali janga hili la corona, waandishi wengi wa Habari kote duniani wanakabiliwa na tishio kubwa , unyanyasaji na mashambulizi kwa kutekelezwa wajibu wao, huku waandishi karibu 60 wakiuawa mwaka jana pekee.
Ameongeza kuwa wanawake mara nyingi wanalengwa akitolea mfano wa mwandishi wa Colombia Jineth Bedoya Lima mshini wa tuzo yam waka 2020 ya siku ya uhuru wa vyombo vya Habari duniani.
Wengine amewataka kuwa ni Maria Ressa mshindi wa tuzo ya Habari za utafiti kutoka Ufilipinoambaye ni mwanzilishi mwenza wa wavuti wa Rappler.