Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uamuzi wa mahakama ya katiba Uganda ni sahihi:OHCHR

Fred Kanyike mjasiriamali ambaye anatumia mashine kukamua juisi ya miwa na kuajiri vijana wengine katika viunga vya mji mkuu wa Uganda, Kampala.
UN News/ John Kibego
Fred Kanyike mjasiriamali ambaye anatumia mashine kukamua juisi ya miwa na kuajiri vijana wengine katika viunga vya mji mkuu wa Uganda, Kampala.

Uamuzi wa mahakama ya katiba Uganda ni sahihi:OHCHR

Haki za binadamu

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR leo imekaribisha uamuzi wa mahakama ya katiba nchini Uganda ambao umesema matumizi ya nguvu yaliyoruhusiwa kwa polisi nchini humo kuzuia na kusitisha mikutano ya umma ni kinyume na katiba.

Taariya ya ofisi hiyo iliyotolewa na msemaji wake Rupert Colville hii leo mjini Geneva Uswisi imesema uamuzi huo uliotolewa Alhamisi na mahakama ya katiba unahusiana na sheria ya udhibiti wa umma ya mwaka 2013.

Mtandao wa haki za binadamu nchini Uganda uliwasilisha kesi dhidi ya mwanasheria mkuu wa serikali ukipinga kifungu namba 8 cha sheria hiyo ambacho kiliwapa polisi uhuru wa kutumia nguvu kufunga na kuzuia mikutano yoyote ambayo inachukuliwa kuwa inakiuka utulivu wa umma.

Kwa mujibu wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa uamuzi huo wa mahakama ya katiba ni hatua kubwa na chanya ya maendeleo na inaenda sanjari na wajibu wa Uganda chini ya sheria za kimataifa wa kuruhusu wananchi kuhurahia uhuru wao wa msingi.