Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OHCHR yatiwa wasiwasi na taarifa za watu 15 kunyongwa Misri

Rupert Colville, msemaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu, OHCHR
UN Photo.
Rupert Colville, msemaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu, OHCHR

OHCHR yatiwa wasiwasi na taarifa za watu 15 kunyongwa Misri

Haki za binadamu

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR ina wasiwasi kuhusu taarifa kutoka Misri isemayo watu 15 wamenyongwa mwezi huu wa Februari ambapo watu tisa maisha yao yalikatiliwa isiku ya Jumatano wiki hii huku wengine sita walikabiliwa na hukumu ya kifo mapema mwezi huu.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini, Genenva, Uswisi, msemaji wa ofisi hiyo, Rupert Colville amesema kumekuwa na visa kama hivyo katika miaka ya hivi karibuni huku watu wakihukumiwa katika mazingira kama hayo nchini Misri bila kujali utaratibu wa kisheria

Bwana Colville amesema, “mauji hayo ni ya hukumu ya kifo ambayo inakubalika chini ya sheria za kimataifa lakini Umoja wa Mataifa kama mjuavyo unachagiza utokomezwaji wa hukumu ya kifo, lakini tatizo hapa ni hukumu ya haki, kuteswa, kulazimishwa kukiri na kadhalika.

Kwa mujibu wa ofisi ya haki za binadamu, watu kadhaa wamehukumiwa hukumu ya kifo na kuna hatari kubwa ya wao kuuwawa baada ya kukabiliwa na mashtaka ya unyanyasaji

Ofisi hiyo imetoa wito kwa mamlaka nchini Misri kusitisha utekelezaji wa hukumu hizo  ikiongeza kuwa licha ya kwamba hukumu ya juu kabisa inakubalika lakini ni lazima utaratibu wa mahakama uwe wenye haki na ufuate sheria ili kuhakikisha haki inazingatiwa.

Bwana Colville amesema watu tisa walionyongwa Februari 20 walihukumiwa kwa mauaji ya mwendesha mashtaka mkuu Hisham Barakat. Aidha wengine watatu walinyongwa Februari 13 baada ya kuhukumiwa kwa kuua afisa wa polisi, jenerali Nabil Farrag, kwa mujibu wa OHCHR.

Mapema Februari 7, wanaume watutu walinyongwa kufuatia mauji ya mtoto wa kiume wa jaji. Hatua hii inaendena na ile ya awali ambapo OHCHR ilitoa wito kwa Cairo mnamo Januari 2018 kufuatia madai kwamba watu ishirini  walinyongwa katika kipindi cha wiki moja.