Afrika nasi tuna vipaumbele vyetu COP25- PACJA

6 Disemba 2019

Wakati mkutano huo wa COP25 ukiendelea mashirika ya asasi za kiraia kutoka barani Afrika yakiwakilisha nchi zaidi ya 40, chini ya mwamvuli wa Muungano wa Afrika wa haki na tabianchi (PACJA), yamedai jumuiya ya kimataifa kuchapuza mchakato na maamuzi yatakayozingatia mazingira na maslahi ya bara hilo .

Mashirika hayo yamesema maamuzi ni lazima yalionyeshe bara la Afrika kama kanda yenye mazingira na mahitaji maalum kwani makadirio mbalimbali yaliyofanywa na ripoti kuhusu mabadiliko ya tabianchi IPCC yanaonyesha kwamba endapo mwenendo wa sasa utaendelea basi Afrika itakuwa na joto mara 1.5 zaidi ya kiwango cha joto cha wastani cha kimataifa, wakati baadhi ya sehemu za Afrika tayari zinashuhudia nyuzi joto 2ºC, ikiwa ni kiwango kikubwa zaidi ya madirio yaliyowekwa ya nyuzi joto 1.5ºC. 

Miongoni mwa wanaopasa zauti hiyo kwa niaba ya asasi za kiraia ni Fazal Issa mkurugenzi mtendaji kutoka kumbukumbu ya Sokoine Tanzania lakini pia ni mratibu wa makundi tisa  kutoka Afrika ya shirika la Umoja wa Mataifa linalohusiana na masuala ya mazingira UNEP. Akizungumza na UN News Kiswahili ametaja mambo matano ambayo asasi hizo zinayataka yajumuishwe katika maamuzi ya COP25

 

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter