Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wa biashara ni wakati wenu kupiga jeki vita dhidi ya mabadiliko ya tabianchi

Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres akihutubia kikao cha ngazi ya juu kuhusu kutunza tabianchi, kandoni mwa COP25 huko Madrid Hispania leo Desemba 11, 2019
UNFCCC
Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres akihutubia kikao cha ngazi ya juu kuhusu kutunza tabianchi, kandoni mwa COP25 huko Madrid Hispania leo Desemba 11, 2019

Viongozi wa biashara ni wakati wenu kupiga jeki vita dhidi ya mabadiliko ya tabianchi

Tabianchi na mazingira

Muda unayoyoma na kasi ya mabadiliko ya tabianchi inaanza kutupa kisogo tusiposimama imara basi tunaangamiza kizazi hiki na kichacho, ni wakati wa sekta ya biashara kuingia kati katika vita hivi.

Wito huo umetolewa leo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika mkutano wa ngazi ya juu wa mkutano wa 25 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi COP25 mjini Madrid Hispania akiwataka viongozi katika sekta ya biashara kushika usukani na kubadili historia.

“Hii ni nafasi nzuri hususan kwa viongozi wa biashara kubaini njia muhimu za kushiriki katika mbio hizi za kuishinda dharura ya mabadiliko ya tabianchi.”

Ameongeza kuwa mapema mwaka huu, kabla ya mkutano wa G20, mameneja wa mali wanaowakilisha karibu nusu ya mtaji wa uwekezaji duniani takriban dola trilioni 34 waliandika kwa viongozi wa G20 wakitaka hatua za dharura za mabadiliko ya tabianchi na kuwataka kuweka bei ya maana kwenye hewa ukaa na kuach kutoa ruzuku kwa Mafuta ya kisukuku na makaa ya mawe duniani.

Kama tulivyoona katika mkutano wa hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi mnamo Septemba, azma iliyoonyeshwa na viongozi wa sekta za biashara na fedha zinatoa uwezekano wa njia ya matumaini.

Kama biashara zitajitanga na mafuta ya kisukuku inasaidia kutoa ishara za masoko kusaka suluhisho za bunifu.” Wakati tukiwashukuru viongozi hawa tunahitaji wengi Zaidi kujiunga haraka na kuongeza kasi. Kiwango cha mabadiliko ya tabianchi kinaweka hatarini mustakabali wet una maisha tutayoyajua katika sayari hii, kwani mabadiliko ya tabianchi tayari yanaathiri watu, biashara, uchumi na mfumo wa maisha kote ulimwenguni.”

Mwanaharakati kijana wa mazingira Greta Thunberf akihutubia kikao cha ngazi ya juu kuhusu kutunza tabianchi kandoni mwa COP25 huko Madrid Hispania hii leo.
UNFCCC
Mwanaharakati kijana wa mazingira Greta Thunberf akihutubia kikao cha ngazi ya juu kuhusu kutunza tabianchi kandoni mwa COP25 huko Madrid Hispania hii leo.

Tunahitaji mshikamano sasa kuliko wakati mwingie wowote

Katibu Mkuu amesema sasa kuliko wakati mwingine wowote tunahitaji serikali, kanda, miji, biashara na asasi za kiraia kufanya kazi kwa pamoja katika kuelekea lengo moja la kuwa na dunia yenye haki, endelevu na mafanikio.

Amesisitiza kwamba “ili kudhibiti ongezeko la joto duniani kusalia nyuzi joto 1.5, tunahitaji kuunguza hewa ukaa ya viwandani kwa asilimia 45 ifikapo mwaka 2030 na lengo la 2050 la kuwa huru bila hewa ukaa. Hiyo ndio njia pekee ya kufikia malengo ya maendeleo endelevu SDGs.”

Amesema wakati tunashuhudia hatua mbalimbali zikichukuliwa kelekea biashara endelevu haziko karibu au kufikia kiwango chochote kinachohitajika sio mtazamo wa nyongeza bali mtazamo wa mabadiliko. Tunahitaji sekta za biashara kuunga mkono sayansi na kuchukua hatua za haraka katika operesheni zake na mnyororo wa thamani.”

Katibu Mkuu amesema ametiwa moyo kwamba makampuni makubwa 170 tayari yameahidikuweka malengo ya kisayansi yanayoweza kuthibitishwa nayatakayopunguza utoaji wa hewa ukaa sanjari na viwango vya kuhakikisha nyuzi joto inasalia1.5 hapo baadaye kwa kupitia malengo na kampeni ya biashara ya “ Matakwa ya biashara nyuzi joto 1.5” ambayo iko bayana leo hii.

Mafanikio yatakayopatikana

Guterres amesema kwa makampuni kufanya hivyo yatakuwa yanachagiza mbinu mpya za kufanya biashara na kusongesha mabadiliko ya kimfumo kote duniani.

Pia yatakuwa yanatuma ujumbe wa wazi kwa walaji, wawekezaji na serikali kwamba wanadhamiria kuongoza katika mchakato wa uchumi wa dunia kuelekea mustakabali usio na hewa ukaa ifikapo 2050. Amesema pia wakati huohuo jumuiya ya kifedha inazidi kuonyesha fursa za kuelekea uchumi unaojali mazingira.

Kwa sasa Katibu Mkuu amesema wawekezaji wanaomiliki thamani ya takriban dola trilioni 4wameahidi kubadili mfumo wa uwekezaji wao na kuingia usiozalisha hewa ukaa ifikapo 2050 kupitia muungano wa Umoja wa Msataifa wa umiliki wa samani zilizizozalisha hewa ukaa kabisa na masoko yanabadilika Zaidi na Zaidi kila uchao.

Hata hivyo amesisitiza kuwa “biashara na wadau wa fedha hawawezi kutimiza lengo hili peke yao, mwaka 2020 nchi zitawasilisha mikakati iliyoboreshwa ya kitaifa ya mchango wao katika kudhiditi mabadiliko ya tabianchi NDCs. Na tunatarajia kuona mikakati ya kutozalisha kabisa hewa ukaa ifikapo 2050 hasa katika sekta muhimu kama za nishati, viwanda, ujenzi na usafiri.”

Na katika kuunga mkono hatua hizo Guterres ametoa wito kwa viongozi katika sekta binafsi na asasi za kiraia  kuzitia changamoto serikali kutumia fursa hii kuweka bayana sera zao za maendeleo ambazo zitawezesha makampuni kuwekeza katika mustakbalihuru bila hewa ukaa.

Tweet URL

 

Dunia itazama

Katibu Mkuu wa umoja wa Mataifa kubadili mtazamo wa kodi kutoka kwenye kipato hadi kwenye hewa ukaa, kumaliza ruzuku kwenye Mafuta ya kisukuku na kuacha uwekezaji kwenye vituo vya makaa ya mawe ifikapo 2020 ni juhudi ambazo zitanufaisha kutoka kwa biashara na msaada wa sekta ya biashara.

Mamilioni ya watu kote duniani na hususan vijana wanatambua kwamba tunahitajikuchukua hatua sasa ili kufanikiwa kudhibiti athari mbaya zaidi za mabadiliko ya tabianchi. Na hii ndio maana Guterres anasema anatoa wito “kwa viongozi kutoka sekta zote kuwa katika upande sahihi za historia. Heb una tuufanye mwaka 2020 kuwa mwaka tunaoiweka dunia katika mustakabali bora bila hewa ukaa.”