Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya haki za binadamu bado ni mbaya Misri-OHCHR

Ravina Shamdasani, msemaji wa ofisi ya haki za binadamu.
Photo UN Multimedia
Ravina Shamdasani, msemaji wa ofisi ya haki za binadamu.

Hali ya haki za binadamu bado ni mbaya Misri-OHCHR

Haki za binadamu

Hali ya haki za binadamu bado ni mbaya Misri watu wakiendelea kushikiliwa kiholea wakati na baada ya maandamano imesema ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva Uswis.

Kupitia tarifa iliyotolewa na msemaji wa ofisi hiyo Ravina Shamdasan hii leo Kamishina mkuu ameelezea hofu yake kuhusu kuendelea kwa kamatakamata hiyo lakini pia masuala mengine ya ukiuwakwaji haki za binadami kijamii na kiuchumi.”Kwa bahati mbaya kamatakamata hiyo inaendelea na imejumuisha watu kadhaa ambao ni mashuhuri na baadhi ya watu wanaoheshimiwa kutoka asasi za kiraia kwa mfano 12 Oktoba mwaka huu maafisa wa ulinzi walimkamata Esraa Abdelfattah mwaandishi wa Habari na mwanaharakati mashuhuri wa kupigania haki za binadamu mjini Cairo. Alichukuliwa na kupelekwa pasipojulikana ambako imearifiwa alipigwa kwa sababu alikataa kuweka neno lasiri kufungua simu yake ya rununu na kisha inadaiwa alishurutishwa kusimama akiangalia ukuta kwa saa saba baada ya simu yake kufunguliwa kwa lazima kwa kutumia amala za vidole vyake na hivyo ikaruhusu simu yake kupekuliwa na maafisa hao.”

Ameongeza kuwa siku iliyofuata ya Oktoba 13 alifikishwa mbele ya mwendesha mashitaka ambaye alitoa amri ya kumuweka rumande kwa siku 15 ukisubiriwa uchunguzi kuhusu madai ya “kushirikiana na makundi ya kigaidi ili kufikia lengo lake, kuchafua jina na kusambaza tarifa za uongo, pamoja na kutumia vibaya mitandao ya kijamii.” Na siku hiyo hiyo Bi.Abdelfattah alianza mgomo wa kula na hadi sasa bado yuko rumande kwenye jela ya wanawake ya Al-Qanateer.

Wiki mbili kabla ya hapo tarehe 29 Septemner vikosi vya usalama pia vilimtia mbaroni Alaa Abdel mmiliki mashuhuri wa blog na mtetezi wa haki za binadamu ikidaiwa kwamba alikuwa akipata mateso ikiwemo kufuingwa kitambaa machoni, na kulazimishwa kuvua nguo na kusalia na chuki kisha na kuambiwa atembee hivyo gerezani huku akiwa amekabwa shingoni na mikono yake kubanwa nyumba ya mgongo wake.

Siku hiyohiyo pia wakili wa bwana Fattah ambaye ni mawanasheria anayejulikana na kuheshimika na mkurugenzi wa kituo cha Adalah kwa ajili ya uhuru haki za binadamu naye aliswekwa mahabusu wakati akihudhuria mteja wake akihojiwa na polisi. Bwana Fattah na wakili wake El-Bager wote wanatuhjumiwa kwa kuwa wajumbe wa kundi la kigaidi, kwa kufadhili kundi la kigaidi, kusambaza tarifa za uongo na kuweka hatarini usalama wa taifa na pia kutumia mitandao ya kijamii kufanya uhalifu. Na tarehe 9 Oktoba waliongezewa siku zingine 15 za kuendelea kukaa rumande.

Ofisi ya haki za binadamu inasema hii ni mifano ya sehemu ndogo tu ya ukiukwaji wa haki za binadamu unaoendelea Misri.

Unaikumbusha serikali ya Misri kuhusu wajibu wake chini ya sheria za kimataifa kuheshimu na kulinda haki za kila mtu, bila kumtesa au kumfanyia unyawa ambao si vitendo vya kiutu, kumdhalilisha au kumuadhibu kwani hiyo ni haki ya kila mtu isiyo na mjadala.

Pia “Tunatoa wito wa serikali ya Misri kufanyia haraka uchunguzi madai yote ya utesaji, ukiukwaji wa haki za binadamu kwa watu walio mahabusu na kuchukua hatua za kisheria kuhakikisha vitendo hivyo havitokei tena.