Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafua ya nguruwe aina ya Afrika yanasambaa kwa kasi Asia:FAO

Homa ya nguruwe ambayo inaambukiza sana na inaweza kuwa na athari kubwa kwa wafugaji wadogo. (Maktaba Machi 2017)
IAEA/Laura Gil Martinez
Homa ya nguruwe ambayo inaambukiza sana na inaweza kuwa na athari kubwa kwa wafugaji wadogo. (Maktaba Machi 2017)

Mafua ya nguruwe aina ya Afrika yanasambaa kwa kasi Asia:FAO

Afya

Shirika la chakula na kilimo FAO leo limesema mafua yahoma ya nguruwe aina ya Afrika yanasambaa kwa kasi barani Asia na tayari yameshaathiri nchi kadhaa za bara hilo

Takwimu za hivi karibuni za FAO kutoka mashinani zinaonyesha kumekuwa na mlipuko wa homa hiyo nchini Myanmar na sasa umeikumba pia Ufilipino. Hadi sasa zaidi na nguruwe milioni 5 wamekufa na homa hiyo barani Asia au wameuawa ili kuepusha kusambaa zaidi kwa homa hiyo.

Wataalam wa FAO wanasema wanahofia kwamba idadi ya nguruwe walioathirika itaongezeka na hivyo kuonya kwamba hali hiyo itazidisha kutokuwa na uhakika wa chakula katika ukanda wa Asia

Mtaalam wa afya ya wanama wa FAO Juan Lubroth anafafanua zaidi kuhusu hali halisi.

Hakuna chanjo imara dhidi ya homa ya nguruwe.
©FAO/Sue Price
Hakuna chanjo imara dhidi ya homa ya nguruwe.

(SAUTI YA JUAN LUBROTH)

“Sasa ni zaidi ya miezi 12 tangu homa hiyo ya mafua ya nguruwe ya Afrika ilipobainika na kuripotiwa nchini China, na tangu hapo imesambaa katika nchi nyingine kadhaa kwenye ukanda huo Lao, Cambodia, Vietnam, Jamhuri ya watu wa Korea na hivi karibuni mwezi uliopita tumekuwa na visa nchini Myanmar na Ufilipino.”

Na kwa nini FAO inatiwa hofu na mlipuko huo?

(SAUTI YA JUAN LUBROTH )

Tunatiwa hofu kwa sababu matumuzi ya nguruwe na nyama ya nguruwe katika mlo ni muhimu katika mataifa mengi ya Asia, na China ina asilimia 50 ya nguruwe wote wanaofungwa majumbani duniani hivyo kwa hakika tuna tiwa wasiwasi mkubwa na sekta hii ambayo ni muhimu kwa kilimo, kwa usalishaji wa chakula, kwa uhakika wa chakula na kwa biashara ya kimataifa.”