Nilianzisha shirika la kuwasaidia wanawake wajane baada ya mimi mwenyewe kuchungulia kaburi- Dianah Kamande 

16 Agosti 2019

Leo katika mada kwa kina tunamulika kisa cha mwanamke mmoja nchini Kenya ambaye anasimulia madhila ya ukatili wa kiinsia.

Dianah Kamande ni mama wa watoto wawili nchini Kenya ambaye katika mazingira ya kushangaza, siku moja mume wake alirejea nyumbani akiwa na nia moja tu, kumuua mkewe, wanaye wawili na kisha yeye mwenyewe ajiue. Ingawa watoto walitoroshwa haraka, mama yao hakuwa na bahati hiyo kwani alikatwakatwa kwa mapanga kichwani na sehemu nyingi za mwili hivi sasa zimepandikizwa vyuma na mishipa ya bandia. 

Baada ya tukio hilo Dianah amebakia kuwa mjane kwani mume wake alijiua baada ya kufikiri kuwa ameshamuua mkewe. 

Sasa Dianah ameanzisha kundi la kuwaleta pamoja wajane ili wasaidiane katika masuala kadha wa kadha. Flora Nducha alifanya mahojiano na Bi Kamande alipokuwa mjini New York Marekani mapema mwaka huu kuhudhuria kikao cha kimataifa cha hali ya wanawake duniani.  

 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter