Mtaalam wa UN kutathimini hali ya haki za uhuru wa kuandamana na kujumuika Sri Lanka

16 Julai 2019

Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa Clément Nyaletsossi Voule atatembelea Sri Lanka kuanzia tarehe 18 hadi 26 Julai 2019 kwa ajili ya kutathimini hali ya haki za uhuru wa kuandamana kwa amani na kujumuika nchini humo.

Ziara yake imekuja wakati ambapo Sri Lanka imepiga hatua chanya katika juhudi za kupanua mwanya wa sauti ya kiraia, ujenzi wa tasisi thabiti na huru, na hatua muhimu kupata ukweli na maridhaino.

Voule amesema anatumai kuwa ziara yake  itawezesha uthabiti Zaidi wa uhuru wa umma  wakati ambapo nchi hiyo inapitia changamoto lukuki ikiwemo mashambulio ya kigaidi kwenye siku ya Pasaka.

Mjumbe huyo Maalum atatembelea mji mkuu Colombo na mikoa ya Kaskazini, Kusini na Mashariki mwa nchi.

Katika ziara hiyo ya siku tisa pia atakutana na mafisa wa serikali, wawakilishi wa  vyombo vya sharia, bunge, wanahabari, mashirika ya kiraia na vyama vya kibiashara na wale wa Kamisheni ya haki za binadamu ya Sri Lanka.

Pia atakutana na wawakilishi wa mfumo wa Umoja wa Mataifa na mashirika mengine yasio ya kiserikali na wadau wengine nchini humo.

Kando na kutathimini hali ya haki ya uhuru wa kuandamana kwa amani na kujumuika, Voule atatathimini hali ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, tasisi za kulinda haki za umma katika muktadha wa kukabiliana na ugaidi na utungaji sheria kwa dharura na haki ya kutumia mtandao ya intaneti.

Mtaalam huyo atahotubia mkutano wa wanahabari tarehe 26 Julai  kwenye makao ya Umoja wa Mtaifa  mjini Colombo na kutoa ripoti isio ya kina kuhusu tathimini yake.

Atasubiriwa kutoa kutoa ripoti kamili ya ziara hiyo hapo Juni mwaka 2020 kwenye kikao cha 44 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataiafa.

 

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud