Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Eneo huru la biashara Afrika ni chachu ya maendeleo:Amina Mohammed

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed
UN Photo - Jean-Marc Ferre
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed

Eneo huru la biashara Afrika ni chachu ya maendeleo:Amina Mohammed

Ukuaji wa Kiuchumi

Mwishoni mwa wiki naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amina J. Mohammed alihudhuria mkutano wa Muungano wa Afrika  AU na kushiriki uzinduzi na utekelezaji wa kihistoria wa eneo huru la biashara barani humo (AfCFTA).

Bi Mohammed amesema kwa kutia saini kwa Nigeria na Benin kwa makubaliano hayo ya AfCFTA kumelifanya bara la afrika kuwa ndio kubwa zaidi la eneo huru la biashara duniani likiwa nan chi 54 na jumla ya watu bilioni 1.2.

Ameongeza kuwa kuzinduliwa kwa eneo hilo huru la biashara ni chachu kubwa ya maendeleo kwa bara la Afrika. Akiwa Niamey nchini Niger Bi.

Mohammed alikutana na rais wa niger, mwenyekiti wa kamisheni ya Muungano wa afrika, rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Rais wa Gambia, Rais wa Nigeria, Rais wa ethiopia  na rais wa Benki ya maendeleo barani Afrika ADB.

Naibu Katibu Mkuu ameshukuru uhusiani uliopo baina ya Umoja wa Mataifa na bara la Afrika kwa kuendelea kuzichagiza nchi wanachama kutoka barani humo kutumia AfCFTA na kuongeza juhudi katika kusongesha mbele ajenda ya maendeleo ya mwaka 2030 na ajenda ya Afrika ya mwaka 2063.