Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uingereza yapoteza kura ya kuendelea kutawala visiwa vya Chagos:GA

Waziri Mkuu Pravind Kumar wa Mauritius akihuttubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wakati  mjadala wa upigaji kura kuhusu kisiwa cha Chagos
UN Photo/Eskinder Debebe)
Waziri Mkuu Pravind Kumar wa Mauritius akihuttubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wakati mjadala wa upigaji kura kuhusu kisiwa cha Chagos

Uingereza yapoteza kura ya kuendelea kutawala visiwa vya Chagos:GA

Masuala ya UM

Baraza kuu la Umoja wa Matafa leo limeunga mkono mswada unaokosoa hatua ya Uingereza kuendelea kukalia visiwa vya Chagos, vilivyoko baharí ya Hindi na kuagiza visiwa hivyo viunganishwe tena na jirani zake Mauritius  ndani ya miezi sita.

Katika kura kuhusu mswada huo wa uamuzi huo, 116 zilizunga mkono, wajumbe zaidi ya 50 hawakupiga na kura tano tu ndio zilizopinga zikiwemo za Uingereza, Marekani na Hungary. Kura hiyo imefuatia maoni yaliyotolewa na mahakama ya kimataifa ya haki (ICJ) mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu ambnayo yalieleza kwamba  “Uingereza inawajibika kumaliza utawala wake katika visiwa hivyo haraka iwezekanavyo.”

Uingereza iliendelea kushikilia uhuru wa visiwa hivyo baada Mauritius kujinyakulia uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka 1968 kufutia ripoti ya maafikiano ya fidia baina ya mataifa hayo mawili. Jamii nzima ya wanachos waliondolewa kwa nguvu kutoka katika eneo hilo kati ya mwaka 1967 na 1973 na walipigwa marufuku ya kurejea.

Mahakama ya ICJ imesema kwamba kumaliza udhibiti wa Uingereza katika visiwa hivyo ni hatua ya lazima ili kumaliza kabisa ukoloni nchini Mauritius kama njia ya kuhakikisha haki ya watu kujitawala. Visiwa hivyo vinajulikana sana Uingereza kama “Utawala wa Uingereza baharí ya Hindi”

Hata hizo azimio lililopitishwa leo haliilazimishi Uingereza kuchukua hatua , lakini kwa mujibu wa duru za Habari mafanikio hayo katika kura ya leo dhidi ya Uingereza yametokana na kampeni kubwa iliyofanyika kwenye Umoja wa Mataifa na katika makao makuu visiwa hivyo.