Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

katika miaka 10 ijayo, kutakuwa na ajira zaidi ya milioni 2 za ICT wasichana zichangamkieni-ITU

Wasichana walioshiriki kwenye kongamano la kimataifa la wasichana na Habari, Mawasiliano na Teknolojia, ICT  huko Addis Ababa, Ethiopia tarehe 25 Aprili 2019
ITU/M.Tewelde
Wasichana walioshiriki kwenye kongamano la kimataifa la wasichana na Habari, Mawasiliano na Teknolojia, ICT huko Addis Ababa, Ethiopia tarehe 25 Aprili 2019

katika miaka 10 ijayo, kutakuwa na ajira zaidi ya milioni 2 za ICT wasichana zichangamkieni-ITU

Utamaduni na Elimu

Leo hii nchi 170 kote duniani zinaadhimisha siku ya  kimataifa ya wasichana walio kwenye tasnia ya teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT).

Siku hii inatumiwa na Umoja wa Mataifa  kuziba pengo la kijinsia katika ulimwengu wa kidijitali. Lengo likiwa kuhamasisha kizazi kipya cha wasichana kutafuta fursa zaidi katika tasnia ya teknolojia ya mawasiliano.

Muungano wa kimataifa wa Mawasilino ITU unakadiria kuwa katika kipindi cha miaka 10 ijayo, kutakuwa na ajira zaidi ya milioni mbili za teknolojia ambazo haziwezi kujazwa kwa sababu ya ukosefu wa wataalam wa digitali. Kwa wasichana hiyo ni fursa muhimu ambayo wakijiandaa mapema itaweza kuwanufaisha linesema shirika hilo

ITU inasema ujuzi bora wa wasichana unawapa fursa ya kuwa na nafasi za juu katika soko la ajira, mshahara mzuri na pia kuongeza uhamiaji wa kikazi.

Tayari katika nchi mbalimbali wasichana wameanza kwenda na kasi za kubuni njia mbalimbali ambazo zinatumia mitandao. Nchini Tanzania Faraja Nyarandu msichana mchechemshaji amebudi mfumo wa kupata elimu wa kutumia kompyuta ambao unawasaidia wanafunzi kuweza kujifunza mahali popote walipo kwa njia ya mtandao. Faraja anafafanua kjinsi imfumo huo anaouita Shule Direct unavyofanya kazi