Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni kweli maambukizi ya VVU yamepungua Nigeria lakini tusibweteke -UNAIDS.

Wanawake wawili walio na VVU wakiwa wamekaa sakafuni wakipokea ARV dawa ya kupunguza makali kutoka kwa muuguzi.
UNICEF/Shehzad Noorani
Wanawake wawili walio na VVU wakiwa wamekaa sakafuni wakipokea ARV dawa ya kupunguza makali kutoka kwa muuguzi.

Ni kweli maambukizi ya VVU yamepungua Nigeria lakini tusibweteke -UNAIDS.

Afya

Matokeo ya utafiti uliofanywa na serikali ya Nigeria kuhusu maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI, VVU nchini humo, yametangazwa hii leo mjini Abuja Nigeria na Geneva Uswisi na kuonesha kushuka kwa maambukizi kutoka asilimia 2.8 hadi asilimia 1.4 miongoni mwa watu wa umri kuanzia miaka 15 hadi 49.

 Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na UKIMWI, UNAIDS na shirika la kudhibiti UKIMWI nchini Nigeria wanakadiria kuwa kuna watu milioni 1.9 wanaoishi na VVU nchini Nigeria.

Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS Michel Sidibé ameyapokea makadirio mapya katika taarifa ya utafiti huo akisema kuwa ufahamu mzuri wa hali ilivyo nchini humo utawafanya Nigeria kuweza kuwafikia watu wanaoishi na VVU au ambao wako hatarini kupata virusi hivyo, “Ninaipongeza serikali ya Nigeria na wadau kwa kufanya utafiti huu  ambao unatupatia ufahamu mzuri zaidi wa hali ya maambukizi ya VVU katika nchi. Wakati ni habari njema kuwa kuna watu wachache wanaoishi na VVU nchini Nigeria kuliko ilivyofikiriwa mwanzo, hatutakiwi kuweka chini silaha zetu. Hebu tutumie matokeo ya utafiti huu kujipanga vizuri zaidi katika kuzuia VVU, matibabu na huduma kwa watu walio katika uhitaji mkubwa na kuhakikisha Nigeria inakuwa kwenye mstari wa kuumaliza uogonjwa wa UKIMWI ifikapo mwaka 2030”

Dawa za kupunguza makali ya UKIMWI-ARV
Photo: Sean Kimmons/IRIN
Dawa za kupunguza makali ya UKIMWI-ARV

Naye rais Muhammadu Buhari wa Nigeria akizungumza kwenye mji mkuuAbuja Nigeria amepokea habari hiyo kuwa kuna watu wachache wanaoishi na VVU nchini mwake kuliko idadi iliyokuwepo awali nah apo akazindua mpango mkakati wa kitaifa wa kupambana na VVU kwa kipindi cha mwaka 2019 hadi 2021. Katika miaka ya hivi karibuni, Nigeria imepiga hatua nzuri katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI. 

Rais  Buhari amesema, “kwa mara ya kwanza, mwisho wa UKIMWI kuwa  tishio kwa afya kufikia mwaka 2030 unaanza kuonekana. Ninasihi sisi sote tusibweteke bali tuongeze kasi. Heb una tufanye kazi kwa pamoja, kwa ajili ya hatua ya mwisho.”

Wakati maambukizi yanaonekana kuwa asilimia 1.4 miongoni mwa watu wa umri wa miaka 15 hadi 49, wanawake wa umri wa miaka hiyo tajwa wako katika uwezekano mara mbili wa kuwa wanaishi na VVU kuliko wanaume kwa asilimia 1.9 dhidi ya 0.9. Tofauti ya maambuki katika ya wanawake na wanaume ni kubwa miongoni mwa watu wazima wasio na umri mkubwa ambapo kwa upande wa wale wa kike ni kati ya wenye umri wa miaka 20 hadi 24 wakiwa ni mara tatu ya kuwa na uwezekano wa kuwa wanaishi na VVU wakilinganishwa na wale wa kiume wa umri kama huo.

Kwa mujibu wa takwimu mpya, miongoni mwa watoto wa umri wa kuanzia umri 0 hadi miaka 14, maambukizi ya VVU ni asilimia 0.2. Taarifa ya UNAIDS inasema kuwa katika miaka ya hivi karibuni zimefanyika juhudi za kuzuia maambukizi mapya ya VVU kwa watoto.