Wasichana wasiogope sayansi kwa sababu inatuzingira kila mahali- Bi Wahome

11 Februari 2019

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake na wasichana katika sayansi, Shirika la Umoja wa mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UN- Women na lile la  elimu sayansi na utamaduni, UNESCO yamesema sauti za wanawake na wasichana na ujuzi katika sayansi, teknolojia na ubunifu ni muhimu katika kuleta suluhu katika Dunia ya sasa ambayo inashuhudia mabadiliko ikiwemo mabadiliko haribifu.

Halikadhalika mashirika hayo yamesema kuna haja ya kuziba pengo katika sekta ya sayansi, teknolojia, uhandisi na hisibati, STEM na kuimarisha usawa wa kijinsia katika kazi husika.

Kauli hiyo imethibitishwa na Anastasia Wahome, mkuu wa kitengo cha sayansi na takwimu  katika shirika la kikanda la kiserikali linalousika na usimamizi wa rasilimali kwa ajili ya maendeleo lililoko jijini Nairobi, Kenya  akisema kuwa bado wasichana hawajakumbatia masomo ya STEM kama inavyohitajika kwa kuwa wasichana wengi bado wana hofu ya kujifunza masomo hayo kutokana na kukosa watu wa mfano kwao.

Akaenda mbali zaidi na kutoa wito kwa wasichana ambao wangependa kujikitia katika masomo ya sayansi wajitokeze.

 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter