Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua lazima zichukuliwe dhidi ya uonevu kwa watoto na barubaru mtandaoni:UNICEF

UNICEF inachagiza matumizi bora ya intaneti na barubaru huko Dili, Timor-Leste
© UNICEF/UN067579/Gomes
UNICEF inachagiza matumizi bora ya intaneti na barubaru huko Dili, Timor-Leste

Hatua lazima zichukuliwe dhidi ya uonevu kwa watoto na barubaru mtandaoni:UNICEF

Amani na Usalama

Katika kuadhimisha siku ya usalama wa mtandao wa intaneti hii leo, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF limetoa wito wa kuchukuliwa hatua kuzuia uonevu na ukatili mtandaoni kwa zaidi ya asilimia 70 ya vijana kote duniani.

Katika taarifa yake UNICEF imeonya kuhusu hatari zitokanazo na uonevu na ukatili huo kwa barubaru na vijana asilimia 70.6 wenye umri wa kati ya miaka 15 na 24 duniani na kuongeza kuwa ikiwa ni miaka 30 baada ya kupitishwa mkataba kuhusu haki za mtoto ni wakati wa kuelekeza nguvu kwenye haki za kidijitali za watoto.

Wito huo uliotolewa katika Siku ya usalama mtandaoni umekuja kufuatia utafiti uliofanywa na UNICEF ukihusisha vijana na kupokea majibu zaidi ya milioni moja katika kipindi cha wiki tano kutoka nchi zaidi ya 160, na mapendekezo kutoka kwenye mfululizo wa majadiliano ya vijana yajulikanayo kama #ENDviolence yaliyofanyika dunia nzima.

Katika utafiti huo vijana wametoa majibu ya kina kuhusu nini wao na wazazi wao, waalimu na watunga sera wanaweza kufanya ili kuwalinda, na suala la kutenda wema lilijitokeza kama moja ya hatua yenye nguvu na muhimu katika kuzuia uonevu na uonevu mtandaaoni. Akizungunmzia hilo mkurugenzi mtendaji wa UNICEF Henrietta Fore amesema “Tumesikia kutoka kwa watoto na vijana kote ulimwenguni na wanachokisema kiko bayana :Mtandao wa intaneti umekuwa jangwa jema, na ndio sababu katika siku hii ya usalama wa mtanado wa intaneti UNICEF inamkaribisha kila mmoja, vijana na wazee kuwa wema mtandaoni na kutoa wito wa hatua madhubuti kufanya mtandao wa inaneti kuwa mahala salama kwa kila mtu.”

Matumizi ya mtandao

Bi Fore ameongeza kuwa mtandao wa intaneti umekuwa ni sehemu ya maisha ya vijana licha ya kiwango cha uchumi walichonacho.Kwa mujibu wa muungano wa kimataifa wa mawasiliano ITU, wakati asilimia 94 ya vijana wa umri wa kati ya miaka 15-24 katika nchi zilizoendelea wako mtandaoni, Zaidi ya asilimia 65 ya vijana katika nchi zinazoendelea wako mtandaoni.

Hii ni Zaidi ya kasi ya matumizi ya mtandai wa intaneti kwa idadi nyingine ya watu. Na duniani kote nusu ya watu wote bila kujali umri wako mtandaoni.

Hatua hii UNICEF inasema inakuja na ongezeko la hatari, kwani kwa mujibu wa takwimu za shirika la elimu , sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO, kiwango cha waathirika wa uonevu mtandaoni kwa watoto na vijana barubaru katika nchi za kipacho cha juu ni kati ya asilimia 5 hadi 21, huku wasicha wakionekana kuwa wahanga zaidi ya wavulana.

Athari za uonevu mtandaoni

Uonevu mtandaoni unaweza kusababisha athari kubwa kwani unaweza kuwafikia watu wengi zaidi na unaweza kusalia mtandaoni milele, na kuwa jinamizi kwa waathirika katika maisha yao yote. Uonevu na uonevu wa mtandao havitengamani na ni chachu ya taia haribifu. Waathirika wa uonevu mtandaoni mara nyingi wanaweza kutumia pombe na mihadarati na kuhepa shule kuliko wanafunzi wengine.

Na pia wanauwezekano mkubwa wa kupata alama za chini shuleni, kutojiamini na kupata matatizo ya kiafuya. Na katika mazingira mengine ya hatari Zaidi uonevu mtandaoni imesababisha watu kujiua.

Hivyo katika siku ya leo UNICEF inamkumbusha kila mtu kwamba wema  kwenye mtandao nan je ya mtandao ni wajibu ambao unaanza la kila mmoja wetu.

UNICEF inafanya nini?

Na katika kuenzi miaka 30 ya kupitishwa kwa mkataba kuhusu haki za mtoto UNICEF pia inatoa wito wa kufufua haraka ushirikiano wa kuziweka haki za mtoto katika msitari wa mbele kwenye juhudi za masuala ya kidijitali. Na kama sehemu ya hili, UNICEF inatekjeleza miradi kutimiza ahadi ya kuunganisha wat una mtandao wa intaneti na elimu kwa niaba ya Watoto wa dunia hii ikisisitiza kwamba “Ni wakati kwaserikali, familia, wanazuoni na sekta binafsi kuwaweka watoto na vijana katika kitovu cha será za masuala ya kidijitali, kwa kuwalinda na madhila yatokanayo na mtandao wa intaneti na kupanua wigo wa fursa nzuri na kwa mambo mazuri.”

TAGS: UNICEF, mtandao wa intaneti, uonevu, #ENDviolence